Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkenya aliyesafiri Saudia kikazi arejea na watoto wawili wa baba tofauti

4b33017e823b0d1c Mkenya aliyesafiri Saudia kikazi arejea na watoto wawili wa baba tofauti

Tue, 21 Sep 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Mwanamke mmoja Mkenya amesimulia namna alisafiri Saudi Arabia miaka saba iliyopita akiwa na matumaini ya kutengeneza pesa na kuboresha maisha ya wanawe watatu lakini aliishia kurejea nyumbani mikono mitupu akiwa na watoto wengine wawili.

Hata hivyo, maisha nchini Saudia hayakuwa rahisi kama alivyodhania na alirejea nyumbani wiki chache zilizopita akiwa na watoto wawili aliozaa na wanaume tofauti raia waSudan.

Merab Wanjiku alisafiri kutoka Kenya hadi Saudi Arabia akiwa na matumaini kwamba ni nafasi nzuri ya kuboresha maisha ya wanawe Wakati huo alikuwa ameolewa na mwanamume ambaye alikuwa akimdhulumu kimwili na pamoja walijaliwa watoto watatu.

Merab Wanjiku kutoka Gatundu, Kiambu alirejea Kenya siku chache zilizopita, baada ya miaka saba nchini Saudia lakini huzuni ni kwamba kando na kurejea na watoto wengine wawili, hakuwa na lolote la kujivunia.

Akizungumza na Baruthi Wa Thayu kupitia YouTube, mama huyo alisema aliondoka Kenya kwa sababu ya changamoto alizokuwa anakabiliana nazo kwenye ndoa yake.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke