Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkenya Aliyefungwa Gereza la Guantanamo Kuachiliwa Huru Baada ya Miaka 15

RAJABU Mkenya Aliyefungwa Gereza la Guantanamo Kuachiliwa Huru Baada ya Miaka 15

Thu, 13 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkenya Mohammed Malik Bajabu na Guled Hassan Duran, raia wa Somalia, wanatazamiwa kuachiliwa kutoka katika gereza la Guantanamo Bay nchini Cuba. Wawili hao wamekuwa katika gereza la Marekani huko Guantanamo Bay, Cuba, kwa zaidi ya muongo mmoja.

Bajabu amekuwa ikishikiliwa katika gereza hilo tangu 2007 huku Duran akizuiliwa tangu 2006. Kulingana na CNN, wawili hao waliruhusiwa kuachiliwa, kulingana na stakabadhi za umma.

Maamuzi hayo yanajiri wakati gereza hilo likiadhimisha miaka 20 wiki hii tangu lilipofunguliwa chini ya utawala wa George W. Bush.

CNN iliripoti kwamba Rais Joe Biden alisema hadharani kwamba anataka kufunga gereza hilo na Baraza la Usalama la Kitaifa linapitia ukaguzi wa gereza hilo "ili kubaini njia mwafaka ya hatma yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live