Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mke wa rais aliyeondolewa madarakani Gabon afungwa jela - ripoti

Mke Wa Rais Aliyeondolewa Madarakani Gabon Afungwa Jela   Ripoti Mke wa rais aliyeondolewa madarakani Gabon afungwa jela - ripoti

Thu, 12 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Mke wa Rais aliyeondolewa madarakani wa Gabon, Ali Bongo Odimba, amefungwa jela, wakili wake ameliambia shirika la habari la AFP.

Sylvia Bongo, ambaye alikuwa chini ya kifungo cha nyumbani, alituhumiwa kwa ubadhirifu wa fedha za umma.

Mumewe alilazimishwa kuondokai tarehe 30 Agosti.

Wakili Francois Zimeray aliliambia shirika la habari la AFP kwamba kufungwa kwake siku ya Jumatano ni hatua ya "kiholela" na "utaratibu usio halali".

Bi Bongo mwezi uliopita alishtakiwa kwa utakatishaji fedha, kupokea mali ya wizi, kughushi nyaraka.

Mwanawe Noureddin Bongo Valentin pia amefunguliwa mashtaka ya rushwa, ubadhirifu wa fedha na kuwekwa kizuizini kabla ya kesi yake kuanza kusikilizwa.

Jeshi lilichukua mamlaka mara baada ya Ali Bongo kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa rais wa Gabon.

Alikuwa ofisini tangu 2009 alipomrithi babake ambaye alitawala nchi hiyo kwa miaka 41.

Chanzo: Bbc