Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mke wa Tatu wa Mfalme Zwelithini Achaguliwa Kuwa Kiongozi wa Wazulu

Mantfombi MaDlamini Zulu?fit=650%2C430&ssl=1 Mke wa Tatu wa Mfalme Zwelithini Achaguliwa Kuwa Kiongozi wa Wazulu

Fri, 26 Mar 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Mke wa Tatu wa Mfalme Zwelithini Achaguliwa Kuwa Kiongozi wa Wazulu March 26, 2021 by Global Publishers



Familia ya Kifalme ya Zulu nchini Afrika Kusini imemteua Mke wa tatu wa Mfalme Goodwill Zwelithini kushikilia nafasi ya Uongozi hadi pale Mfalme mpya atakapotawazwa.

Malkia Mantfombi Dlamini Zulu ameshikilia wadhifa wa Kimalkia tangu alipoolewa na Mfalme mwaka 1977. Uteuzi wake umeibua mjadala kwamba mmoja wa wanawe atakuwa Mfalme wa Wazulu.

Mfalme Zwelithini (72) alikuwa akiugua maradhi ya Kisukari na alifariki hospitalini kutokana na changamoto za kiafya zilizochochewa na Ugonjwa wa Corona tarehe 12 mwezi Machi. Alikuwa Mfalme kwa karibu miaka 50.

Chanzo: globalpublishers.co.tz