Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mke wa Rais wa Marekani awasili nchini Kenya

Jill Biden.jpeg Mke wa Rais wa Marekani awasili nchini Kenya

Sat, 25 Feb 2023 Chanzo: Bbc

Mke wa Rais wa Marekani, Jill Biden anawasili nchini leo. Katika ziara yake ya siku mbili, atakutana na Mke wa Rais wa Kenya, Rachel Ruto.

Taarifa kutoka ofisi ya Bi.Ruto inasema ziara ya Dkt.Biden inanuiwa kuimarisha ushirikiano wa Marekani na Kenya na bara la Afrika na pia kuendeleza vipaumbele vya pamoja kati ya Marekani na Kenya.

Anatarajiwa kuelekeza umakini wake katika mgogoro wa usalama wa chakula unaoathiri Pembe ya Afrika, inaripoti VoA.

Alianza safari yake wiki hii barani humo kwa kutembelea Namibia, nchi nyingine pekee barani anayotembelea.

Chanzo: Bbc