Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mke wa Rais mstaafu ashitakiwa kwa wizi Zambia

Esther Lungu Mashitaka.jpeg Mke wa Rais mstaafu ashitakiwa kwa wizi Zambia

Tue, 28 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama jijini Lusaka, Zambia imeanza kusikiliza shauri dhidi ya Esther Lungu ambaye ni mke wa Rais Mstaafu, Edgar Lungu, pamoja na polisi wawili.

Esther anakabiliwa na tuhuma za wizi wa magari matatu, wizi wa hatimiliki ya mali jijini Lusaka na kukutwa na dola za Marekani 400,000 ambazo inaaminika ni zao la uhalifu.

Katika kesi hiyo shahidi ameiambia mahakama kuwa mtuhumiwa alichukua kwa nguvu gari lake, hatimiliki ya nyumba yake na magari mawili ya mwanae.

Hata hivyo watuhumiwa hao walikana mashitaka hayo walipokamatwa kwa mara ya kwanza Septemba mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live