Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mke wa Pili Azua Kioja Mazishini Akitaka Mwili wa Mumewe

Ab537649e3c22fc1 Mke wa Pili Azua Kioja Mazishini Akitaka Mwili wa Mumewe

Tue, 6 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Ubishi ulizuka kutokana na pale ambapo mwili wa mrehemu Lolii Angela ungelezwa kati ya boa la mke wa kwanza au wa pili

- Mke wa kwanza wa marehemu aliaga dunia ila kulingana na tamaduni za Waturkana alipaswa alazwe kando yake

- Hata hivyo mke wa pili alienda kortini akitaka ruhusa ya kumzika mumewe

Polisi huko Nakwamekwi, kaunti ya Turkana, walikabiliana na waombolezaji na kuishurutisha familia moja kumzika mpendwa wao chini ya ulinzi mkali.

Ubishi ulizuka kutokana na pame ambapo mwili wa marehemu mhandisi Lawrence Lolii Angela ungezikwa kai ya boa la mke wake wa kwanza na yule wa pili.

Mkewe wa kwanza aliaga dunia awali, lakini bado, malumbano yakaibuka kuhusu mila na utamaduni wa Turkana ambapo wazee walaimuru kwamba Lolii azikwe karibu na mkewe wa kwanza.

Hata hivyo, mke wa pili aliyetambulika kama Esther alielekea mahakamani akitaka kuruhusiwa kuuzika mwili wa mumewe ombi ambalo lilikubaliwa.

Mazishi ya mhandisi huyo mwenye umri wa miaka 54 yalishuhudia kizazaa na kuwalazimu maafisa wa usalama kuingilia kati.

Baadaye marehemu alizikwa katika boma la Estehr chini ya ulinzi mkali.

Watoto wa mke a kwanza walilalamika kufungiwa nje ya mipango ya mazishi ya baba yao na hata kuuona mwili wake tangu alipoaga dunia mwezi mmoja uliopita.

Kwenye taarifa sawia na hiyo, kulikuwa na mzozo katika Kanisa la All Saints huko Nakasero, jiji la Kampala nchini Uganda wakati jamaa walipigania mwili wa wakili aliyeaga dunia Bob Kasango Jumanne, Machi 2, asubuhi.

Mabashino makali yaliibuka wakati wa ibada ya mazishi ya merehemu baina ya pande pili kuanza kuzozania mwili wake huku waombolezaji wakisalia midomo wazi.

Kuligana na ripoti jamaa wa kutoka upande wa mkewe walikabiliana na wale wa upande wa wazazi wake huku familia ya mke ikiunyakua mwili wa mwendazake.

Mke wa Kasango, Nice Bitarabeho Kasango na mtoto wake wa kwanza Samora Paul Kasango walizidiwa nguvu wakati mwili huo ukipakizwa kwenye lori ambalo liliondoka kwa kasi eneo la tukio.

Mamake Rose Kabise alisema kuwa hangeweza kuruhusu mwanawe kuzikwa nyumbani kwake mkewe ilhali ni yeye alimlea.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke