Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mke wa Makamu wa rais apata ajali

Samira Bawumia Asd Mke wa Makamu wa rais apata ajali

Mon, 15 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msafara wa mke wa Makamu wa Rais wa Ghana, Samira Bawumia umepata ajali mbaya siku ya juzi Januari 13, 2024 na kusababisha kifo cha mtu mmoja ambaye alikuwa ni mlinzi wake.

Ajali hiyo imetokea katika eneo la Ohene-Nkwanta katika Barabara Kuu ya Accra- Kumasi na kuthibitishwa na mamlaka za usalama nchini humo ,Taarifa zinaeleza kuwa gari dogo lilivamia msafara huo na kuligonga kidogo gari alilokuwa amepanda mke wa makamu wa rais kisha kuligonga vibaya gari lililokuwa nyuma ya gari alilopanda mwanamama huyo.

Licha ya Video za ajali kuonesha jinsi ajali ilivyokuwa mbaya, mke wa makamu wa rais alitoka salama ingawa mmoja kati ya walinzi wake waliokuwa kwenye gari la nyuma yake, amepoteza maisha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live