Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mke apata mfadhaiko baada ya kumzika mtu aliyedhani ni mumewe

CASKET Mke apata mfadhaiko baada ya kumzika mtu aliyedhani ni mumewe

Tue, 7 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamke mmoja Afrika Kusini amelazimika kufanya mazishi ya mume wake mara mbili aliyekufa kwa ugonjwa wa Covid-19 baada ya kubainika kwamba mwili wake ulitambuliwa makosa.

"Walikataa kuniruhusu nione mwili wa mpendwa wangu katika chumba cha kuhifadhia maiti kwasababu ya kanuni za kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19. Sasa nimemzika mtu mwengine."

Hayo ndio yalikuwa maneno ya kusikitisha ya mke wake baada ya kubainika kwamba mwili wa mume wake, 79, umechanganyika na wa mwengine.

Micheal Vukile Noda, kutoka Uitenhage, mashariki mwa Cape alianza kuonesha dalili za ugonjwa wa Covid-19 na hali yake ilipoanza kuzorota mke wake akatafuta matibabu Juni 16. Mara ya mwisho familia yake kumuona ni pale alipobebwa na gari la kubebea wagonjwa akipelekwa hospitali.

Kulingana na mke wa Vukile, Nomsa Noda, 69, alikuwa na mafua kwa muda wa wiki mbili.

"Alienda kumuona daktari lakini hakumaliza matibabu kwasababu alilazwa kabla ya kumaliza dawa," anasema.

Hali yake ilibadilika na akapelekwa kitengo cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi, anasema.

Hospitali iliarifu familia kwamba amepata maambukizi ya mapafu.

Baadae alihamishwa hadi wadi ya wagonjwa wa kawaida na kuwa huko kwa wiki moja.

"Kwasababu hatukuruhusiwa kumtembelea, mara nyingi tulizungumza kwa simu. Lakini kadiri tulivyokuwa tunaendelea kuzungumza, alionekana kuwa dhaifu na mchovu sana hata kuongea ilikuwa shida. Ikafika kipindi ikawa hawezi hata kujibu simu zake unapompigia," amesema Nomsa.

Nomsa aliendelea kuwasiliana na wauguzi kuhusu hali ya mgonjwa wake lakini kila wakati walikuwa wanamuarifu kwamba mume wake yuko salama.

"Jumapili ya siku ya Baba Duniani, nilipiga simu hospitalini kujua vile mgonjwa wangu anavyoendelea na wakaniarifu kwamba yuko salama. Nikawauliza ikiwa matokeo yake ya vipimo vya ugonjwa wa Covid-19 yametoka na wakaniarifu kwamba bado."

Lakini Jumatatu, Juni 22, Nomsa alipokea simu karibia kumi na mbili kasorobo asubuhi na kuarifiwa kwamba mume wake aliaga dunia Juni 21, baada ya kupatikana na ugonjwa wa Covid-19.

Familia haikuruhusiwa kuona au kutambua mwili wa mpendwa wao na ukahamishwa hadi chumba cha kuhifadhi maiti.

"Niliwauliza ikiwa matokeo ya vipimo vya ugonjwa wa Covid-19 yametoka, wakasema ndio na amepatikana nao."

Familia ikaelekea hospitali kuchukua vitu vyake na wakafahamishwa namna ya kuvinyunyizia dawa.

Mlinzi aliwachukulia vibaya kiasi cha kuwatolea ukali na kuwataka kurejea nyuma kupanga foleni ndefu licha ya kwamba tayari walikuwa hapo mapema.

Kile tu walichotakikana kufanya ni kutia saini na kuchukua vitu vya Bwana Vukile. Lakini kwa jinsi alivyofanyiwa, Nomsa alijipata akibubujikwa na machozi.

"Siamini kama mume wangu alikufa kwa ugonjwa wa Covid-19 kwahiyo nikamuomba daktari kama ninaweza kuona matokeo. Mume wangu Vukile na jina tulilooneshwa lilikuwa ni 'Vuyile', kwa hiyo pengine liliandikwa vibaya. Hatukupewa nakala ya matokeo hata baada ya kuitisha."

Walirejea nyumbani na kutoa taarifa walizopewa kwa familia na mazishi yakafanyika Juni 28. Familia na watu wa kanisa kote nchini humo walishiriki na kutoa heshima zao za mwisho.

Ibada hiyo ilikuwa moja kwa moja kupitia mtandao wa Zoom. Wote waliohudhuria moja kwa moja au kupitia njia ya mtandao walionesha hisia zao wakati wanatazama mazishi ikiwemo kuzikwa.

Lakini kile ambacho hawakuwa wanakifahamu ni kwamba sanduku walilodhani kwamba lina mpendwa wao lina mtu mwengine wasiyemfahamu. 'Walishindwa kutuarifu moja kwa moja kilichotokea'

Julai 1, mhubiri mmoja kutoka kanisa la eneo akapitia nyumbani kwake akiwa ameandamana na wahudumu wawili wanaoshughulika na mazishi hospitalini.

"Kwanza mhubiri alioamba kisha tukatiwa kuwa kimya. Na hapo ndipo walipotuarifu kwamba tumemzika mtu mwengine wala sio jamaa wetu," anakumbuka.

Walipouliza hilo limetokea vipi, wahudumu hao walisema wamepigiwa simu kutoka hospitali na kuarifiwa kwamba familia ya mtu aliyezikwa na familia ya Noda hawakuweza kumpata mpendwa wao.

"Wakaangalia maiti zilizotoka Jumapili na kubaini kwamba Vukile Noda bado yuko chumba cha kuhifadhia maiti. Kila mmoja alishtuka na kupata mfadhaiko na hisia zikaanza upya."

Nomsa alisisitiza kwamba anataka kuutambua mwili wa mume wake kuhakikisha kwamba kweli ni yeye na akaruhusiwa.

"Alhamisi Julai 2, walikwenda hospitali kutazama mwili na moja kwa moja wakaelekea makaburini kuuzika kwa mara ya pili."

Nomsa anasema kwamba sio kila mmoja alifanikiwa kufika kwa mazishi sahihi huku familia kidogo tu ikihudhuria.

"Mazishi ya pili yalikuwa na watu kidogo sana kwasababu tayari karibu asilimia 80 ya waombolezaji walikuwa wameshasafiri kurejea makwao wakidhania kwamba wametoa heshima zao za mwishi mwa mume wangu. Kuwapigia n akuwaomba warejee tena kwa mazishi sahihi ingekuwa kutojali wengine, mke wake amesema."

Noda alisema wahudumu wakushughulikia mazishi walifahamu mkanganyiko uliotokea Jumanne lakini walishindwa kupata ujasiri na kuwaarifu moja kwa moja

Baada ya mazishi, familia ilipokea simu kutoka kwa wahudumu wa masuala ya mazishi kuwaarifu kwamba maafisa wa idara ya afya wangependa kuwatembelea kuomba msahama rasmi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live