Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'Mkataba wa nipe nikupe na China hauifaidishi DRC' - Tshisekedi

'Mkataba Wa Nipe Nikupe Na China Hauifaidishi DRC'   Tshisekedi 'Mkataba wa nipe nikupe na China hauifaidishi DRC' - Tshisekedi

Wed, 24 May 2023 Chanzo: Bbc

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inasema China haizingatii masharti ya mkataba wake na DRC wenye thamani ya mabilioni ya dola za kimarekani uliotiwa saini mwaka wa 2008.

Serikali ya Kinshasa inasema kuwa mkataba huo haukueleweka na unailaghai nchi hii, hivyo inataka uangaliwe upya.

Rais Félix Tshisekedi atawasili Beijing siku ya Jumatano, ambapo yeye na kundi kubwa la maafisa wataanza ziara ya siku tano.

Imepangwa kuwa atakutana na mwenzake Xi Jinping siku ya Ijumaa, katika ziara yake atatembelea pia miji ya Shenzhen, Shanghai na Hong-Kong, na kutakuwa na mijadala mbalimbali kuhusu ushirikiano mwingine kati ya China na DR Congo.

Balozi Zhu Jing wa China mjini Kinshasa alisema "natumai kuwa ziara hii itakuwa na tija na kuleta nguvu mpya ya ushirikiano".

Ni hivi tu karibuni ambapo serikali ya Kinshasa imeonyesha kutofurahishwa na jinsi makubaliano yaliyofanywa na China miaka 15 iliyopita hayana faida kwa nchi hii na kwamba "China haifanyi kile ilichokubali".

Katika tangazo lake wiki iliyopita baada ya kikao cha baraza la mawaziri, Tshisekedi aliwaambia wajumbe wa serikali kwamba kamati inayohusika na utafiti wa mkataba huu imetoa imekamilisha tathmini yake , ambayo itasaidia katika mazungumzo na China katika siku zijazo.

Mkataba ukoje?

Huu ni mkopo unaoitwa wa 'karne', ambao Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) lilijaribu kusitisha mwaka 2009 kwa sababu ya deni kubwa ambalo tayari DRC inalo kwa taasisi za fedha za Magharibi, lakini Kinshasa na Beijing zimesimama kidete na kuendelea, kulingana na na gazeti la Ufaransa Le Monde Diplomatique.

Mwaka 2008, Kinshasa na Beijing zilitiliana saini makubaliano ya ‘nipe mimi’ ambapo ilikubaliwa kuwa China itafadhili miradi ya miundombinu yenye thamani ya dola bilioni 6, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara za lami zenye urefu wa kilomita 3,500, ujenzi wa kilomita 380 za reli, hospitali 32. na vituo vya afya 145 na zaidi...

Kwa upande mwingine, Kongo pia inaipa China migodi yake, hasa ya shaba na kobalti yenye thamani ya tani milioni 10 kwa mwaka, pamoja na misamaha ya kodi kwa uagizaji na mauzo ya nje.

Kufuatia mkataba huu, kampuni ya SICOMINES pia ilianzishwa, China ikimiliki 62% na DR Congo ikimiliki 32% - hisa zenyewe hazijafurahisha vyama vya upinzani na mashirika ya kiraia ya Kongo.

Ofisi ya Rais Tshisekedi inasema kwamba anaenda China kwa mwaliko wa mwenzake Xi Jinping, na baadhi ya wachambuzi wanasema kuwa Tshisekedi anataka makubaliano haya yabadilike na hiyo ndiyo sababu kuu ya yeye kwenda.

Chanzo: Bbc