Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkataba wa nafaka wa Ukraine kuzingatia mataifa ya Afrika

Mkataba Wa Nafaka Wa Ukraine Kuzingatia Mataifa Ya Afrika Mkataba wa nafaka wa Ukraine kuzingatia mataifa ya Afrika

Thu, 3 Nov 2022 Chanzo: Bbc

Rais wa Uturuki amesema makubaliano ya kukomesha mauzo ya nafaka kutoka Ukraine yatazingatia mataifa ya Afrika yanayokabiliwa na njaa.

Recep Tayyip Erdogan alisema yeye na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy wamejadiliana kupeleka nafaka katika nchi za Afrika.

"Hali ya Djibouti, Somalia na Sudan si nzuri hata kidogo. Iwapo kutakuwa na tatizo katika nchi nyingine ambazo hazijaendelea, tutafanya usafirishaji hadi nchi hizi," Bw Erdogan alisema katika mahojiano na kituo cha utangazaji cha Uturuki ATV.

Mkataba huo wa nafaka uliratibiwa na Umoja wa Mataifa na Uturuki mwezi Julai, na hivyo kuhitimisha mzingiro wa miezi mitano wa Urusi dhidi ya bandari za Ukraine ambao ulinasa mamilioni ya tani za nafaka na mafuta ya alizeti na kusababisha bei ya vyakula kupanda.

Mkataba huo unamalizika tarehe 19 Novemba na wale wanaohusika bado wanapaswa kukubaliana kurefusha muda huo.

Urusi ilikuwa imesitisha uungwaji mkono wa mauzo ya nafaka lakini ilikubali wiki hii kuanza tena ushiriki wake katika makubaliano hayo.

Chanzo: Bbc