Mjumbe maalum wa mkuu wa jeshi la Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan amekutana na Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini kujadili njia za kumaliza vita huko Khartoum.
Rais Kiir alichaguliwa na Jumuiya ya kikanda, Igad, kuongoza juhudi za upatanishi ili kusitisha mapigano kati ya jeshi la Sudan na Wanajeshi wa Msaada wa Dharura (RSF).
Lakini uamuzi wa pande zinazozozana kuhudhuria mazungumzo ya kusitisha mapigano nchini Saudi Arabia umechochea uvumi kwamba juhudi za upatanishi za kikanda zimepuuzwa.
Katika mkutano na waandishi wa habari katika mji mkuu wa Sudan Kusini Juba, Dafalla al-Haj Ali alijaribu kuzungumzia wasiwasi huo, akisema alitaka kusema "kwa kwa sauti ya juu " kwamba Igad haijatengwa.
"Tuna imani kamili na Rais Salva Kiir," aliongeza.
Bw Kiir alisisitiza umuhimu wa mzozo huo kumalizika, na kusema kwamba hakuna nchi yoyote inapaswa kuchukua fursa hiyo kuidhoofisha Sudan.