Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mjumbe wa EU azuiwa kuingia kwenye ubalozi wa Ufaransa Niger

Mjumbe Wa EU Azuiwa Kuingia Kwenye Ubalozi Wa Ufaransa Niger Mjumbe wa EU azuiwa kuingia kwenye ubalozi wa Ufaransa Niger

Thu, 7 Sep 2023 Chanzo: Bbc

Umoja wa Ulaya umepinga vikali baada ya balozi wake nchini Niger Salvador Pinto da França kuzuiwa kuingia katika ubalozi wa Ufaransa katika mji mkuu Niamey.

"Umoja wa Ulaya unashutumu na unasikitikia vikwazo vya uhuru wa kutembea ambavyo balozi wa Ulaya, aliyeko Niamey, alikuwa mwathirika Jumanne hii Septemba 5, alipokuwa akienda kwa ubalozi wa Ufaransa," msemaji wa EU Nabila Massrali alisema.

"Chini ya Mkataba wa Vienna wa 1961, balozi wa Umoja wa Ulaya ameidhinishwa ipasavyo na ni lazima, kwa hiyo, aweze kutekeleza dhamira yake kwa heshima kamili ya mkataba huo," aliongeza.

Ubalozi wa Ufaransa umezuiwa baada ya utawala wa kijeshi kuamuru kukamatwa na kufukuzwa kwa balozi wa Ufaransa Sylvain Itté, lakini amekataa kuondoka.

Wanajeshi hao walitoa amri hiyo tarehe 26 Agosti kulipiza kisasi kwa Paris kukataa kumtambua kiongozi wa mapinduzi Jenerali Abdourahmane Tchiani na kusisitiza kumtambua tu Rais aliyeondolewa madarakani Mohamed Bazoum kama rais halali wa Niger.

EU imeita amri ya kufukuzwa "uchochezi mpya ambao hauwezi kusaidia kupata suluhisho la kidiplomasia kwa mzozo uliopo".

Chanzo: Bbc