Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mjukuu wa Moi atakiwa kupalilia mbegu alizopanda na kuhepa

6bec4460feb9f369 Mjukuu wa Moi atakiwa kupalilia mbegu alizopanda na kuhepa

Mon, 10 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Toroitich anadaiwa kuhepa majukumu ya kuwalea watoto wawili aliopata na mpenzi wake miaka nane iliyopita

- Jeruto alisema Toroitich alihepa majukumu ya kuwalea watoto wao wenye umri wa miaka 9 na 11

- Si mara ya kwanza kwa Toroitich kuandamwa na mkono wa sheria kwani 2016 alifikishwa Nakuru akidaiwa kuiba simu mbili katika ASK Show

Mjukuu wa aliyekuwa rais Daniel Moi anaandamwa na mkono wa sheria baada ya kudaiwa kuhepa majukumu ya ulezi.

Collins Toroitich amefikishwa mahakamani na aliyekuwa mpenzi wake akitakiwa kulipia majukumu ya ulezi wa watoto wake wawili.

Gladys Jeruto Tagi alisema Toroitich, ambaye ni mtoto wa Jonathan Toroitich, amehepa majukumu ya kuwalea watoto wao wenye umri wa miaka 9 na 11.

Kulingana na taarifa iliyochapishwa na jarida la Nation, Tagi kupitia wakili wake David Mongeri anataka kijana huyo aamrishwe na mahakama kumpa KSh 1M kila mwezi.

Alisema watoto hao wanahitaji fedha hizo ili kupata chakula, kodi ya nyumba, karo na pia wapate kiposhi cha kujivinjari.

Mbele hakimu Benjamin Limo Tagi anasema licha ya kuwa Toroitich ni kutoka familia nzito kimfuko, alimwachia majukumu ya watoto hao miaka minane iliyopita na huwa hampi hata sumni.

Ainataka mahakama kumsaidia akilia kuwa hana kazi rasmi ila hutegemea vibarua kujikimu pamoja na watoto hao.

Si mara ya kwanza kwa mjkuu huyo wa Moi kujipata pabaya kwani 2016 alikuwa mbele ya mahakama ya Nakuru kwa kesi ya wizi wa simu.

Alikuwa ameshtakiwa kwa wizi wa simu mbili kutoka kwa kina dada wawili mwezi Julai.

Alifikishwa mbele ya hakimu mkuu David Kemei, Toroitich alidaiwa kuiba simu hizo wakati wa hafla katika ASK show.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke