Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mji huu Niger ndio chimbo la wakambizi wanaokwenda Ulaya

Wahamiajiii Morocco Tena.png Mji huu Niger ndio chimbo la wakambizi wanaokwenda Ulaya

Thu, 2 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maidani ya usafiri wa umma katika mji wa Agadez huko kaskazini mwa Niger imekuwa ikishuhudia wimbi la watu wanaowasili na kuondoka tangu utawala wa kijeshi wa nchi hiyo ubatilishe amri ya kupiga marufuku usafirishaji wa wahamiaji haramu na shughuli zote zinazohusiana na wahajiri huko Niger Novemba mwaka jana.

Ripoti zinasema kuwa biashara haramu ya kuwavusha wahamiaji imerejea kwa kasi hivi sasa ambapo misafara ya raia wa Kiafrika wanaotaka kuelekea katika nchi za Ulaya imekuwa ikiondoka Jumanne na Alhamisi kila wiki katika mji wa Agadez huko kaskazini mwa Niger.

Huku wakisaidiwa na mawakala wao kuwavusha raia wa Kiafrika wanaotaka kuhajiri Ulaya; wahusika wa biashara hiyo huondoka Agadez kwa magari madogo aina ya 4X4 au kwa kutumia malori kuelekea Libya au Algeria nchi ijirani na Niger. Libya na Ageria huwa ni kituo cha mwisho cha wahajiri hao kabla ya kuvuka bahari hadi Ulaya.

Sadio Diallo raia wa Senegal anayetaka kwenda Ulaya anasema hivi na hapa ninamnukuu:" Lengo langu nikifika Ulaya ni kujiunga na jeshi la Ufaransa, kwa sababu nataka kwenda Ufaransa, kama nilivyokuwa mwanajeshi huko Senegal. Napendelea nitakapofika Ulaya kuendelea na utumishi wangu (jeshini).

Tangu kufunguliwa kwa Agadez, wahamiaji wasiopungua 5,000 tayari wamepita katika mji huo wakielekea Libya na Algeria wakiwa na matumaini kwamba watavuka bahari ya Mediterania na kuingia Ulaya.” Wahajiri wa Kiafrika katika Bahari ya Mediterania

Chehu Azizou Mratibu wa Mradi kwa jina la "Alarmephone Sahara Project" ameeleza kuwa, kwa mwezi kumekuwa na takriban safari tatu hadi tano kutoka Agadez kwenda Libya huku kila safari ikibeba watu wapatao 2,000.

Naye Alice Fereday mchambuzi wa ngazi ya juu wa Mpango wa Kupambana na Jinai za Kitaifa Zilizoratibiwa anasema kuwa wahamiaji hao wanaojaribu kuelekea Ulaya wanakabiliwa na hatari nyingi ikiwa ni pamoja na hatari za kukamatwa na kuwekwa kizuizini.

Si hayo tu, bali wahajiri hao wa Kiafrika wamekuwa wakipoteza maisha pia wakiwa baharini kutokana na sababu mbalimbali kabla hata ya kuwasili Ulaya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live