Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mjane wa TB Joshua avunja kimya na ujumbe wa huzuni akimuomboleza mumewe

168b5a6864b54f53 Mjane wa TB Joshua avunja kimya na ujumbe wa huzuni akimuomboleza mumewe

Mon, 7 Jun 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Kifo cha mhubiri maarufu wa Nigeria TB Joshua Juni 5, 2021, kiliwashtua wengi

- TB Joshua alivuma bara Afrika na mataifa yanayozungumza Latin

- Wafuasi wake walifurika kutoa rambi rambi zao wakimuelezea marehemu kama mtu mcha Mungu ambaye alimtumkia na moyo wote

- Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari pia aliomboleza pamoja na familia na waumini wa Kanisa la Synagogue of All Nations kufuatia kifo cha TB Joshua

Evelyn Joshua, mjane wa mwasisi wa kanisa la Synagogue Church of All Nations, TB Joshua, amevunja kimya chake kuhusu kifo cha mume wake.

Siku ya Jumapili, Juni 6, mama huyo wa watoto alionyesha hisia zake za huzuni kufuatia kifo cha ghafla cha mume wake.

Katika ujumbe ambao TUKO.co.ke umeona, Evelyn alichapisha ujumbe wa huzuni akimuomboleza mume wake akisema kuwa ni Mungu pekee anaweza kuwatuliza waliofiwa.

''Kumpoteza mpendwa si rahisi. Haijalishi ikiwa ghafla ama kutabiriwa huwa ya kuvunja moyo.Huzuni yaweza kutulemaza na ndio maana ni muhimu kukaa ndani ya Mwenyezi Mungu. Ni yeye pekee anaweza kuondoa machungu yote ya moyoni na kututuliza wakati huu. Tafuta hifadhi kwake," aliandika.

Wafuasi wake walifurika kutoa rambi rambi zao wakimuelezea marehemu kama mtu mcha Mungu ambaye alimtumkia na moyo wote.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari pia aliomboleza pamoja na familia na waumini wa Kanisa la Synagogue of All Nations kufuatia kifo cha TB Joshua.

Daily Nation iliripotia kuwa Joshua alikamilisha ibada haraka isivyokuwa kawaida baada ya kuanza kuhisi mgonjwa jioni ya Jumamosi, Juni 5.

Kisha aliondoka kanisani na kuelekea nyumbani kwake baada ya ibada iliyokuwa imeanza saa kumi na mbili jioni.

Hata hivyo, waumini walikuwa na wasiwasi baada yake kukosa kurejea kanisani punde walivyotarajia.

Walikwenda kumtafuta na kumpata amefariki.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke