Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mjane wa Rais Aliyeuawa Arejea Haiti

119475885 Aa245317 4253 45dc A434 Af414ba9e4ab?fit=800%2C335&ssl=1 Mjane wa Rais Aliyeuawa Arejea Haiti

Sun, 18 Jul 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Mjane wa Rais Aliyeuawa Arejea Haiti July 18, 2021 by cshechambo



MJANE wa rais aliyeuawa Haiti, Jovenel Moise amerudi nyumbani baada ya kutibiwa majeraha aliyoyapata katika shambulio.

Waziri wa mawasiliano wa serikali Frantz Exantus kupitia mtandao wa twitter ameandika kwamba Martine Moise, alipokelewa katika uwanja wa ndege wa Port-au-Prince na waziri mkuu wa mpito Claude Joseph.

Martine alilazwa katika hospitali ya Miami huko Florida nchini Marekani kwa siku 10 baada ya kushambuliwa pamoja na mumewe nyumbani kwao ambapo rais huyo aliuawa kwa kupingwa risasi mnamo Julai 7.

Mazishi ya kiongozi huyo yanatarajiwa kufanyika tarehe 23 huko Cap-Haitien, jiji la kihistoria, kaskazini mwa Haiti, ambalo limeathirika vibaya na machafuko tangu kuuwawa kwa Moise.

Share this:TweetWhatsApp Related

Chanzo: globalpublishers.co.tz