Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mjane wa Papa Shirandula alia baada ya Jalang'o kuahidi kumsomesha bintiye

A5ebcee85f5ef967 W Mjane wa Papa Shirandula alia baada ya Jalang'o kuahidi kumsomesha bintiye

Mon, 19 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Wahusika wa mchezo wa Papa Shirandula walifanya hafla ya kumbukumbu katika Hoteli ya Azure, Nairobi kumkumbuka mwendazakeBeatrice Andega, mjane wa Shirandula alitoa hotuba ya huzuni akimkumbuka mume wakeAlipokuwa akizungumza, alizidiwa na hisia baada ya Jalang'o, Captain Otoyo na Njoroge kujitokeza kumsaidia binti yakeAndega alisema alikuwa anakumbwa na msongo wa mawazo kwa sababu ya kushindwa kulipa karo ya binti yake Sherry Owendi

Mnamo Julai 18, 2021, ndio inatimia mwaka mmoja baada ya kifo cha Charles Bukeko, maarufu Papa Shirandula. Shirandula aliangamizwa na COVID-19.

Wahusika wa mchezo wa Papa Shirandula walifanya hafla ya kumbukumbu katika Hoteli ya Azure, Nairobi kumkumbuka mwendazake.

Juma Anderson, ambaye aliigiza kama bosi wa Shirandula, Wilbroda mkewe wa kuigiza, Awinja mpwa wake, Kawira, Njoro na mke wake wa kuigiza Wafirethi, Otos naJalas walikuwa miongoni mwa waliohudhuria hafla hiyo.



Read also

Mimi Siwezi Kuolewa na Mwanamume Maskini, Asema Mwimbaji Justina Syokau

Beatrice Andega, mjane wa Shirandula alitoa hotuba ya huzuni akimkumbuka mume wake na alipokuwa akizungumza, alizidiwa na hisia baada ya Jalang'o, Captain Otoyo na Njoroge kujitokeza kumsaidia binti yake.

Andega alisema alikuwa anakumbwa na msongo wa mawazo kwa sababu ya kushindwa kulipa karo ya binti yake Sherry Owendi, ambaye anasomea katika shule ya Moi Educational Centre. Yuko katika Gredi ya Tano.

Jalang'o na wenzake waliahidi kulipa karo ya mtoto huyo hadi chuo kikuu.

"Kuna shida ambazo unashindwa namna utazitatua lakini namshukuru Mungu kwa sababu ni Mungu mwenye majibu. Kile ambacho Jalang'o amefanya kimegusa moyo wangu sana.Ni wiki moja sasa nilikuwa nafikiria karo. Mungu ametoa jawabu," alisema mjane huyo huku akimwaga machozi.

Mambo yalikwenda sambamba kwene hafa hiyo na watu wengine wa familia walisema waliurahia kutambua kuwa hata kaburini, Papa Shirandula badi anapendwa.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke