Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mjane atumia teknolojia kujifungua mtoto

8963a110b5117612 Mjane atumia teknolojia kujifungua mtoto

Thu, 8 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Sarah alimpoteza mume wake Scott kutokana na mshtuko wa moyo kabla ya wawili hao kupata mwanao wa kwanza Kwa bahati nzuri wawili hao walikuwa wamehitimisha utaratibu wa mbolea ya kiinitete na Sarah alipata mimba Scott akiwa marehemuPia ana matumaini kuwa anatatumia mchakato huo kupata mtoto wa pili kupitia yai moja lenye mbolea lililosalia hospitalini

Sarah Shellenberger mwenye umri wa miaka 40, hivi majuzi alijifungua mtoto wa mume wake marehemu miezi 14, baada ya kumpoteza.

Sarah alimpoteza mume wake Scott kutokana na mshtuko wa moyo lakini aliweza kubeba mimba yake kupitia kwa njia ya mbolea ya kiinitete.

Kulingana naye, mwanawe Hayes mwenye miezi miwili ameponya uchungu wa moyo wake baada ya kumpoteza Scott.

“Nikimshika Hayes amekuwa dawa yangu na ameponya moyo wangu katika njia nyingi,” alisema mwalimu huyo wa Oklahoma kama alivyonukuliwa na The Mirror.

Kupata mtoto wa piliSarah na Scott walikuwa wamekamilisha utaratibu wa mbolea ya kiinitete wakati profesa huyo wa sayansi alipatwa na mshutuko wa moyo akifunza chuoni.

Akitambua kuwa mume wake angelipenda wawe na watoto, alipata mimba miezi sita baada ya kifo cha Scott akitumia kiinitete kilichohifadhiwa.

Sarah pia ana matumaini kuwa atatumia mchakato huo kupata mtoto wa pili kupitia yai moja lenye mbolea lililosalia hospitalini.



Sarah na Scott walianza kuchumbiana mwaka 2017, mapenzi ambayo yaliwapelekea kuvalishana pete ya uchumba miezi minne baadaye na kuoana rasmi Septemba 2018.

Wakiwa katika ndoa, walihangaika sana kupata mtoto licha ya kuwa na matimaini ya kuzaa angalau watoto watatu na hapo ndipo daktari aliwashauri kutimia mbinu ya upandikizaji (IVF).

Kifo cha ScottSiku chache baada ya kufuata ushauri huo, Scott alipatwa na mshtuko wa moyo na alilazwa katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi(ICU) lakini alishindwa kurejesha fahamu.

Wakati alipokea taarifa kuwa mume wake hawezi tena kuwa hai, Sarah alishtuka kwa sababu Scott alikuwa buheri wa afya.

Japo ana furaha, Sara anajutia kuwa Scott hakupata nafasi ya kukutana na mwanao.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke