Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mizozo yaathiri mauzo ya bidhaa za Kenya nchini Tanzania na Uganda

Mizozo Yaathiri Mauzo Ya Bidhaa Za Kenya Nchini Tanzania Na Uganda Mizozo yaathiri mauzo ya bidhaa za Kenya nchini Tanzania na Uganda

Mon, 22 Jan 2024 Chanzo: Bbc

Mauzo ya Kenya kwa nchi jirani za Uganda na Tanzania yamepungua tangu Oktoba mwaka jana huku kukiwa na uhusiano mbaya kati ya nchi hizo tatu za Afrika mashariki, tovuti inayomilikiwa na watu binafsi ya Kenyans.co.ke iliripoti jana.

Takwimu kutoka Ofisi ya Takwimu ya Kenya (KNBS) zilionyesha kuwa mauzo ya Kenya hadi Uganda yalipungua kutoka $61.5m hadi $49.2 kati ya Septemba na Oktoba 2023, huku mauzo ya nje ya Tanzania yakishuka kutoka $35.7m hadi $31.4m katika kipindi hicho, tovuti ilisema.

Kenya imekanusha kuwa uhusiano wake na nchi hizo mbili umedorora tangu Rais William Ruto aingie madarakani Septemba 2022.

Licha ya kukanusha, Uganda imeishtaki Kenya kwa madai ya kuinyima leseni ya kuagiza mafuta kupitia bandari ya Mombasa.

Tanzania ilipiga marufuku kwa muda safari za shirika la ndege la Kenya Airways kati ya Nairobi na Dar es Salaam mapema mwezi huu ili kulipiza kisasi uamuzi wa Nairobi kunyima haki ya Air Tanzania kuendesha safari za mizigo kati ya nchi hizo mbili.

Chanzo: Bbc