Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mitandao ya kijamii kufungwa Uganda

Mtanzanianews 137341589 443031030391499 2957254891527957261 N 660x400 Mitandao ya kijamii kufungwa Uganda

Wed, 13 Jan 2021 Chanzo: millardayo.com

Uganda imeagiza watoaji huduma za mtandao kufunga mitandao yote ya kijamii na programu za kutuma ujumbe kufikia Jumanne hadi wakati usiojulikana.

Kwa mujibu wa barua kutoka kwa mdhibiti wa mawasiliano nchini humo iliyonukuliwa na shirika la habari la Reuters.

Imeeleza kuwa watumiaji walikuwa wamelalamika, kwamba hawataweza kupata mtandao wa Facebook na WhatsApp, majukwaa ya mitandao ya kijamii yanayotumiwa sana katika kipindi cha kampeni kabla ya uchaguzi wa urais kwenye nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

“Tume ya mawasiliano Uganda inaagiza kusitisha ufikiwaji na utumiaji wa moja kwa moja au kinyume chake, kwa mitandao yote ya kijamii pamoja na programu za kutuma ujumbe mitandaoni hadi siku isiyojulikana,” imeeleza sehemu ya hiyo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa tume hiyo.

Aidha, Msemaji wa tume hiyo, Ibrahim Bbossa na Msemaji wa serikali, Ofwono Opondo hawakujibu simu walizokuwa wanapigiwa ili kutoa maoni yao kuhusiana na hilo.

Chanzo: millardayo.com