Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Misururu mirefu yashuhudiwa kwasababu ya uhaba wa mafuta Malawi

Misururu Mirefu Yashuhudiwa Kwasababu Ya Uhaba Wa Mafuta Malawi Misururu mirefu yashuhudiwa kwasababu ya uhaba wa mafuta Malawi

Thu, 20 Jul 2023 Chanzo: Bbc

Mdhibiti wa nishati nchini Malawi anasema nchi hiyo imemaliza akiba yake ya mafuta hasa kutokana na ukosefu wa fedha za kigeni.

Vituo vya mafuta katika mji mkuu wa kiuchumi wa Malawi, Blantyre vina uhaba mpya wa mafuta nchini humo wiki hii.

Misururu mirefu ya madereva wanasubiri kwa saa kadhaa wakati mwingine usiku kucha kwa matumaini ya kujaza mafuta magari yao huku gharama za usafiri wa umma zimeongezeka maradufu.

Mdhibiti wa nishati nchini Malawi anasema nchi hiyo imemaliza akiba yake ya mafuta hasa kutokana na ukosefu wa fedha za kigeni.

Tatizo hilo lilidhihirika wazi siku ya Jumapili wakati madereva wa magari walipoanza kuhangaika kutafuta petroli ingawa dizeli bado ilikuwa inapatikana.

Sasa bidhaa zote mbili zimeisha. Mistari mirefu baadhi ya umbali wa kilomita nzima kutoka kituo cha mafuta imekuwa jambo la kawaida na kupelekea uvumi mwingi kutoka kwa madereva kama Labani Chirwa.

Lakini serikali imeupinga uvumi huo. Hii ni mara ya kwanza tangu mwezi Machi hali ya usambazaji wa mafuta kufikia viwango vya hatari.

Uhaba wa mafuta umewalazimu waendeshaji wa magari ya uchukuzi wa umma kupandisha gharama karibu mara mbili ya nauli zao.

Hata hivyo waendeshaji hao wanasema licha ya kupanda kwa nauli hawapati faida yoyote kwa sababu wanatumia siku moja au mbili kupanga foleni ya mafuta bila kufanya biashara yoyote.

Calisto Kambani anamiliki biashara ya mabasi madogo mjini Blantyre anasema watu wengi hapa wanategemea mabasi madogo. Kwa hiyo tatizo hili limetuathiri sana kwa sababu hata familia zetu zinaishi kwa sababu ya biashara hii na uhaba wa mafuta ni pigo kubwa kwetu.

Malawi imekuwa ikikabiliwa na uhaba wa mafuta wa mara kwa mara tangu mwezi Agosti mwaka jana kwa kiasi kikubwa kutokana na kwamba nchi hiyo haina fedha za kigeni za kutosha.

Benki Kuu ya Malawi ilisema mwezi Juni kwamba akiba ya serikali ya fedha za kigeni haitoshi kudumu hata kwa mwezi mmoja.

Henry Kachaje ni afisa mkuu mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati Malawi.

Aliwaambia waandishi wa habari Jumanne kwamba Malawi haiwezi kuendana na kupanda kwa bei za kimataifa kwa bidhaa za petroli.

Kachaje amesema mdhibiti wa nishati anashirikiana na wauzaji mafuta ili kupunguza uhaba huo.

Kachaje amesema kama yote yatafanyika kulingana na mipango hifadhi ya kimkakati ya mafuta nchini Malawi itarejeshwa tena mwishoni mwa mwezi Agosti.

Alisema uhaba wa mafuta uliopo ni wa muda na anakadiria kuwa utasuluhishwa ndani ya siku tatu.

Chanzo: Bbc