Taasisi ya Kitaifa ya Lishe nchini Misri imetoa wito kwa watu kula miguu ya kuku badala ya nyama kutokana na gharama ya miguu ya kuku kuwa nafuu zaidi, hatua iliyowakasirisha wananchi wengi wakidai ni alama ya umasikini uliokithiri nchi humo.
Kwa mujibu wa ripoti, nchi hiyo ya Afrika Kaskazini inakabiliwa na mfumuko wa bei mbaya zaidi katika kipindi cha miaka mitano, hivyo kusababisha Wamisri wengi kushindwa kumudu kuku ambacho ni chakula kikuu.
Kwa mujibu wa CNN, bei ya kuku imepanda kutoka pauni 30 za Misri (TZS 4,442) kwa kilo mwaka 2021 hadi kufikia pauni 70 za Misri (TZS 5,517)
Uchumi wa Misri ulipata pigo kubwa katika miaka miwili iliyopita wakati athari za janga la UVIKO-19 pamoja na vita vya Ukraine ambavyo vilipunguza akiba yake ya fedha za kigeni, na kupanda kwa bei ya mafuta kulifanya mfumuko wa bei kuongezeka zaidi.