Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Misri yarejesha uhusiano na Uturuki wakati wa ziara ya Erdogan Cairo

Misri Yarejesha Uhusiano Na Uturuki Wakati Wa Ziara Ya Erdogan Cairo Misri yarejesha uhusiano na Uturuki wakati wa ziara ya Erdogan Cairo

Thu, 15 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na mwenzake wa Misri Abdel Fattah al-Sisi wametangaza kufunguliwa kwa mwanzo mpya wa uhusiano baada ya miaka kumi.

Nchi hizo mbili zilikata uhusiano mwaka wa 2013 baada ya Bw Sisi, aliyekuwa waziri wa ulinzi, kumuondoa madarakani Rais wa Kiislamu Mohamed Morsi, mshirika wa Ankara.

Katika mkutano wa pamoja mjini Cairo siku ya Jumatano, viongozi hao wawili walisema wanaanzisha upya uhusiano wao.

Ilikuwa ni ziara ya kwanza ya kiongozi huyo wa Uturuki nchini Misri katika zaidi ya miaka 10.

Makubaliano kadhaa ya nchi mbili yalitiwa saini wakati wa mkutano huo.

Viongozi hao wawili pia wamekosoa mwenendo wa Israel wa vita katika Ukanda wa Gaza na kutaka kusitishwa kwa mapigano.

Chanzo: Bbc