Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Misri yamuachilia huru mwandishi wa Al Jazeera baada ya miaka minne

Mwandishi Wa Al Jazira Misri yamuachilia huru mwandishi wa Al Jazeera baada ya miaka minne

Tue, 2 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwandishi wa habari wa Shirika la Al Jazeera ameachiliwa huru kutoka gerezani nchini Misri, miaka minne baada ya kukamatwa, limesema shirika hilo lenye makao yake Qatar.

Hisham Abdel Aziz alikamatwa maka 2019, kwa akishukiwa kuwa mfuasi wa kikundi cha ugaidi . Alikuwa akiachiliwa huru mara kwa mara na kukamatwa tena.

Al Jazeera iliinukuu familia ya Bw Aziz, ikisema kuwa amerejea nyumbani mjiniCairo.

Ni mmoja wa wafanyakazi kadhaa wa Al Jazeera waliokamatwa nchini Misri tangu utawala wa sasa ulipoingia mamlakani mwaka 2013.

Mwezi Julai mwaka ule, aliyekuwa rais wakati huo, Mohammed Morsi, walipinduliwa kufuatia maandamano makubwa ya kupinga utawala wake.

Makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema tangu wakati huo maelfu ya watu wamekuwa wakikamatwa.

Wengi wamekuwa wakishutumiwa kuwa na uhusiano na vuguvugu lililopigwa marufuku nchini Misri la Undugu wa Kiislamu - Islamist Muslim Brotherhood, ambalo Misri imeishutumu Al Jazeera kuliunga mkono.

Kulingana na Al Jazeera, Bw Abdel Aziz alikamatwa katika uwanja wa ndege wa Cairo alipowasili kutoka Qatar, ambako alikuwa akiishi. Alikuwa njiani kuitembelea familia yake, ilisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live