Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Misri yahutumiwa kuwatesa wanawake kwa madai ya kuwa na uhusiano na IS

Misri Yahutumiwa Kuwatesa Wanawake Kwa Madai Ya Kuwa Na Uhusiano Na IS Misri yahutumiwa kuwatesa wanawake kwa madai ya kuwa na uhusiano na IS

Wed, 17 May 2023 Chanzo: Voa

Mashirika mawili ya haki za binadamu yameshutumu mamlaka ya Misri kwa kuwaweka kizuizini kiholela - na katika baadhi ya matukio kuwatesa - wanawake na wasichana wanaohusiana na washukiwa wa kundi la Islamic State (IS).

Human Rights Watch na Taasisi ya Sinai ya Haki za Kibinadamu zinasema kuzuiliwa huko mara nyingi kunaonekana kutumika kuweka shinikizo kwa wanafamilia wanaoshukiwa kuwa na uhusiano na wanajihadi wa Misri wanaohusishwa na IS.

Mawakili na mashahidi waliohojiwa kwa ripoti hiyo wanasema lengo lilikuwa kutoa habari juu ya washukiwa wa kijihadi au kuwafanya wajisalimishe.

Ripoti hiyo inasema baadhi ya wanawake na wasichana walikuwa waathiriwa wa kundi linalohusishwa na IS.

Chanzo: Voa