Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Misri yaendelea kupinga kuondoshwa wapalestina kutoka ardhi yao

Misri Yaendelea Kupinga Kuondoshwa Wapalestina Kutoka Ardhi Yao Misri yaendelea kupinga kuondoshwa wapalestina kutoka ardhi yao

Fri, 17 Nov 2023 Chanzo: Voa

Waziri wa mambo ya nje wa Misri Sameh Shokr amesema kwamba mawasiliano katika Hamasi na Misri bado yanaendelea, na serikali yake inaendeleza juhudi hizo pia na washirika wengine kimaaifa ili kuwaachilia huru mateka walipo katika ukanda wa Gaza.

Alhamisi jioni akiwa kwenye kikako maalumu na waandishi wa habari wanaoripotia mashirika ya habari ya kigeni, Waziri Shokr akijibu swali linaloangazia uvumi wa kuwa Israel na Marekani zinaishinikiza nchi yake kukubali suala la kuhamishwa raia wa Palestina waliopo katika ukanda wa Gaza ili Misri ifutiwe madeni.

Shokr amekanusha kuwepo kwa jambo hilo na ni taarifa zisizo sahihi, akiongezea kuwa haiwezekani kuwaondosha raia hao nje ya ardhi yao, akitilia mkazo juu ya kadhia hii Waziri Shokri amesema: “Tunatumai kuwa juhudi zetu zitapelekea kuachiliwa kwa haraka mateka”

Katika taarifa za awali Israel ililiripoti kuwa Wapiganaji wa Hamas waliwakamata raia wake 240 wakati wa shambulio la kushtukiza kwenye ya walowezi wake yanayoizunguka Gaza tarehe 7 mwezi Oktoba.

Mapigano ukanda wa Gaza

Hadi kufikia siku ya alhamisi mashambulizi ya Israel katika ukanda wa Gaza yameshafikia siku 41, wanajeshi wa Israel wameendelea kushambulia ukanda huo wakiwasaka na kukabiliana na wapiganaji wa Hamas huku wakisababisha vifo vya raia wasio na hatia ambapo idadi yake ni zaidi ya 11,000 kufuatia athari za mabomu ya moja kwa moja hali ambayo inatajwa kuwa ni ukikwaji wa kanuni za kimataifa na uvunjaji wa haki za raia wa Palestina.

Kwa mujibu wa afisa wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa ni kwamba kuna juhudi zinafanyika ili kuihamisha hospitali ya Al Shifaa ambayo imevamiwa na wanajeshi wa Israel katika ukanda wa Gaza lakini bado vikwazo vya kiusalama vinakwamisha juhudi hizo.

Rick Brennan mkurugenzi katika idara ya dharura ya WHO kwenye ukanda huo ameongeza kusema kuwa shirika la msaada la Hilali Nyekundu ndani ya Palestina nalo pia halina mafuta ya kuendesha gari za wagonjwa kutoka sehemu moja hadi nyingine ndani ya Gaza, na ama kwa upande wa Misri magari yapo ya kuwahamisha wagonjwa licha pia bado kunakosekana dhamana ya usalama njiani.

Chanzo: Voa