Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Misri na UN zajadiliana mgogoro wa Syria na njia za kuutatua

Misriiiii Un Un Misri na UN zajadiliana mgogoro wa Syria na njia za kuutatua

Tue, 22 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sameh Shoukry, Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri na Geir O. Pedersen, Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika kadhia ya Syria wamefanya mazungumzo na kujadiliana matukio yanayoendelea nchini Syria na njia za kuyatatua.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri imesema katika taarifa yake kwamba, miongoni mwa masuala waliyojadiliana wawili hao ni matokeo ya mkutano wa kwanza wa Kamati ya Uhusiano ya Mawaziri wa Nchi za Kiarabu kuhusu Syria, ambao ulifanyika tarehe 15 Agosti mjini Cairo.

Kamati hiyo ambayo iliundwa na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu Arab League, inajumuisha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Saudi Arabia, Jordan, Iraq, Lebanon na mkuu wa Arab League.

Sameh Shoukry amesisitizia nia ya kamati hiyo ya kuupatia suluhu ya kudumu mgogoro wa Syria, kulindwa umoja wa ardhi ya nchi hiyo na kudumishwa utulivu nchini humo.

Shoukry na Pedersen wamekubaliana pia kukutana tena pembeni mwa mikutano ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ifikapo mwezi Septemba mwaka huu.

Baada ya kupita takriban miaka 12 ya kusimamishwa uanachama, hatimaye mwezi Mei mwaka huu, Syria ilirejeshewa uanachama wake katika Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) yenye makao yake mjini Cairo Misri. Rais Bashr al Assad wa Syria aliposhiriki katika mkutano wa Arab Legue nchini Saudi Arabia mwezi Mei 2023

Uanachama wa Syria wa Arab League ulisitishwa mwishoni mwa mwaka 2011 wakati mzozo wa Syria ulipozuka, jambo ambalo lilipelekea baadhi ya mataifa ya Kiarabu kuwaita tena mabalozi wao kutoka Damascus, hatua ambayo ilipingwa vikali na uongozi wa Syria.

Suala la Syria kurejea kwenye Jumuiya ya Nchi za Kiarabu limezifurahisha pande nyingi za ndani na nje ya eneo la ulimwengu wa Kiislamu na Kiarabu na limeonesha jinsi muqawama wa wananchi wa Syria na serikali yao ulivyolilinda taifa hilo la Kiarabu na Kiislamu na kulikoa mbele ya njama za kikatili za maadui.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live