Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Misri lawamani vita Israel na Palestina

Wapalestina 4,651 Wameuawa Katika Vita Misri lawamani vita Israel na Palestina

Sun, 29 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wataalamu na wachambuzi mbalimbali wameendelea kutoa lawama kali dhidi ya serikali ya Rais Abdel Fattah el Sisi wa Misri kwa msimamo dhaifu inaoonesha mbele ya jinai za kuchumpa mipaka zinazofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi wa Ghaza.

Shirika la habari la IRNA limeripoti leo Jumamosi kwamba, wataalamu na wachambuzi wa mambo wa Misri wanalalamikia vizuizi vingi vinavyowekwa na serikali ya nchi hiyo vinavyozuia kuungwa mkono wananchi wa Palesitna na kuilaumu vikali serikali ya Jenerali Abdel Fattah el Sisi kwa hatua zake hizo.

Wimbi kubwa la uungaji mkono wa walimwengu kwa wananchi madhlumu wa Palestina hasa wa Ukanda wa Ghaza liliongezeka sambamba na kuanza jinai za kinyama za Israel dhidi ya Wapalestina tarehe 7 Oktoba 2023 na hadi leo hii maandamano yanaendelea katika kona mbalimbali za dunia kulaani jinai hizo.

Wananchi wa nchi mbalimbali za Kiislamu na Kiarabu wameonesha msimamo mzuri katika kulaani jinai kubwa za Wazayuni ambazo hazijawahi kutokea katika karne ya 21 na wengi wao wana hamu ya kuona wanasahilishiwa mambo ya kuweza kuwasaidia ndugu zao wa Ukanda wa Ghaza.

Wahanga wakubwa wa jinai za Israel huko Ghaza ni watoto wadogo. Wataalamu wanawalaumu viongozi wa nchi za Kiarabu kwa nmsimamo dhaifu wanaoonesha

Inafaa kuashiria hapa kuwa katika kukabiliana na jinai za Wazayuni, vikosi vya muqawama au wapigania ukombozi wa Palestina vilianzisha operesheni ya #Kimbunga_cha_al-Aqsa huko Ukanda wa Ghaza dhidi ya ngome za utawala wa Kizayuni wa Israel kuanzia Jumamosi, Oktoba 7, 2023.

Tangu ilipoanza operesheni hiyo, jeshi la Kizayuni, ambalo halina uwezo wa kukabiliana na wanamapambano wa Palestina, limekuwa likishambulia kwa mabomu maeneo ya raia, hospitali, vituo vya kidini na skuli huko Ghaza.

Wakati huo huo Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza kuwa Wapalestina waliouawa shahidi imeongezeka pia katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na imefikia 110 na wengine zaidi ya 1,900 kujeruhiwa tangu tarehe 7 Oktoba 2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live