Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Misri kuwezesha uhamisho wa watu 7,000 wa kigeni kutoka Gaza

Misri Kuwezesha Uhamisho Wa Watu 7,000 Wa Kigeni Kutoka Gaza Misri kuwezesha uhamisho wa watu 7,000 wa kigeni kutoka Gaza

Thu, 2 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Misri inataka kuwezesha uhamisho wa wageni 7,000 walio na uraia kutoka nchi 60 huko Gaza kupitia kivuko cha ardhini cha Rafah.

Hatua hiyo ilijadiliwa wakati wa mkutano uliofanyika na maafisa wa Misri na mabalozi na wawakilishi wa nchi za nje jana, Jumatano.

Mamlaka ya Palestina ilichapisha orodha ya pili ya majina ya takribani raia 600 wa kigeni, wakiwemo raia 400 wa Marekani, ambao wataruhusiwa kuvuka kuingia Misri kuanzia leo.

Misri pia ilijadili maandalizi ya kupokea Wapalestina waliojeruhiwa na juhudi za Misri kuleta msaada.

Misri ilipokea Wapalestina 46 waliojeruhiwa kati ya 81, ambao walihamishiwa katika hospitali za Sheikh Zuweid, Al-Arish, na Bir Al-Abd.

Kivuko cha Rafah kilifunguliwa jana, Jumatano, kwa idadi ndogo ya majeruhi, wageni, na wenye hati za kusafiria za kigeni kuvuka, kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa vita.

Chanzo: Bbc