Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Misri kunufaika na haya kundi la Brics

Brics Misri.jpeg Misri kunufaika na haya kundi la Brics

Sat, 26 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hatua ya Misri na nchi nyingine tano kukubaliwa kuwa wanachama wapya wa kundi la BRICS kumepokewa kwa hisia tofauti.

Misri, pamoja na nchi nyingine tano za Iran, Saudi Arabia, Muungano wa Falme za Kiarabu, Ethiopia na Argentina juzi Alkhamisi zilikubaliwa kuwa wanachama wapya wa kundi la BRICS ambalo linaundwa na herufi za kwanza za majina ya Kiingereza ya nchi waasisi wa kundi hilo ambazo ni Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini.

Akionesha hisia zake kufuatia kukubaliwa Misri kuwa mwanachama wa BRICS, Gamal Bayoumi, mkuu wa Muungano wa Wawekezaji Waarabu wenye makao yake makuu mjini Cairo amesema: "Kundi hilo litasaidia Misri kuendelea na harakati zake za kukomboa uchumi, kupanua masoko, na kuongeza mauzo ya nje."

Kabla ya nchi hizo sita kukubaliwa kuwa wanachama wapya, idadi ya watu wa nchi za BRICS ilikuwa inafikia asilimia 40 ya watu wote duniani na pato la nchi hizo kimataifa lilikuwa ni robo nzima ya pato la nchi za dunia.

Kukubaliwa Iran kuwa mwanachama wa kundi la BRICS pia kumepokewa kwa furaha na nchi rafiki na kwa wasiwasi mkubwa na maadui ambazo zinasema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni muungaji mkono mkubwa wa ukombozi wa taifa la Palestina na kwamba kukubaliwa kuwa mwanachama wa kundi la BRICS ni ushindi kwa kambi ya muqawama.

Kwa upande wake, Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alisema kuwa mara baada ya kuwasili hapa Tehran kutoka kwenye mkutano wa kundi la BRICS huko Jonnesburg Afrika Kusini kwamba, muungano wa kimataifa una nafasi na machango muhimu katika ushirikiano wa kiuchumi na kibiadhara duniani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live