Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Misri haitaruhusu vitisho kwa Somalia: Rais al Sisi

Misri Haitaruhusu Vitisho Kwa Somalia: Rais Al Sisi Misri haitaruhusu vitisho kwa Somalia: Rais al Sisi

Mon, 22 Jan 2024 Chanzo: Bbc

Rais wa Misri Abdul Fattah al-Sisi amesema makubaliano ya kuipa Ethiopia usafiri wa baharini kupitia Somaliland "hayakubaliki na mtu yeyote".

Akizungumza mjini Cairo karibu na Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud, Bw Sisi alisema Misri haitaruhusu usalama wa Somalia kuhatarishwa.

"Sisi hatutasita kuwaunga mkono ndugu zetu, na ikiwa watatuomba, hatutasita kuchukua hatua," Bw Sisi aliongeza.

Lakini siku ya Jumapili, mshauri wa masuala ya usalama wa taifa wa Ethiopia Redwan Hussein alisema makubaliano yenye utata ya kuifikia Bahari ya shamu yalikusudiwa kwa ajili ya ushirikiano, na sio "kunyakua" au "kudhania kuwa na mamlaka juu ya eneo la nchi yoyote".

Katika taarifa yake katika mtandao wa X, Bw Hussein alisema Ethiopia na Somalia "sio tu majirani walio na mpaka mmoja lakini pia ni mataifa yenye undugu yanayozungumza lugha moja, utamaduni na watu".

"Hatima yetu imeunganishwa na haiwezi kutenganishwa," aliongeza.

Somalia inaiona Somaliland kama eneo lake, na inasema mpango huo ni kinyume cha sheria.

Misri, kwa upande wake, imekuwa na matatizo na Ethiopia kuhusu ujenzi wa Bwawa la Renaissance kwenye Mto Blue Nile, kijito cha Mto Nile, ambayo inautegemea kwa karibu maji yake yote safi.

Chanzo: Bbc