Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Misri haiko tayari kukubali idadi kubwa ya Wapalestina

Misri Haiko Tayari Kukubali Idadi Kubwa Ya Wapalestina Misri haiko tayari kukubali idadi kubwa ya Wapalestina

Wed, 18 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza anatarajiwa kuzuru Misri hivi karibuni.

Wakati wa mzozo huu kumekuwa na mawazo yanayozunguka kwamba Israel inataka kuwahamisha wakazi wa Gaza milioni 2.3 hadi jangwa la Sinai nchini Misri.

Walihutubiwa katika mkutano wa waandishi wa habari na rais wa Misri hapo awali.

"Kinachotokea sasa huko Gaza ni jaribio la kuwalazimisha wakazi kukimbilia na kuhamia Misri, jambo ambalo halipaswi kukubaliwa," Abdul Fattah al-Sisi alisema.

Alionya kwamba kama haya yangetokea, watu wa Misri wanaweza "kutoka nje na kuandamana kwa mamilioni."

Cairo tayari imeonya kwamba ikiwa Wapalestina wataondoka katika ardhi yao, inaweza "kuondoa" matumaini ya Wapalestina ya kuwa taifa.

Lakini pia itakuwa hatari sana kwa serikali ya Misri kama ingeonekana kuhusika katika mpango wowote kama huo- na kuwasha hasira ya umma katika ulimwengu wa Kiarabu.

Mmiminiko wowote wa watu pia ungezidisha mzozo wa sasa wa kiuchumi wa Misri na kuibua hofu ya usalama katika eneo lake lenye utulivu la Sinai.

Sisi alipendekeza kwamba kwa vile Gaza iko chini ya udhibiti wa Israel, Wapalestina wanaweza badala yake kuhamishiwa kwenye jangwa la Negev la Israel wakati wa mashambulizi yake dhidi ya Hamas "hadi wanamgambo hao watakaposhughulikiwa".

Mamia ya malori ya msaada yameegeshwa kaskazini mwa Sinai, yakingoja makubaliano ya kuruhusu kutumwa kupitia kivuko cha Rafah ya Misri kuingia Gaza.

Ni kivuko pekee cha eneo la Palestina ambacho hakidhibitiwi na Israel, lakini kibali cha Israel kitahitajika ili kuruhusu kufunguliwa.

Katika siku za hivi karibuni, kivuko hicho kimeshambuliwa mara nne na mashambulizi ya anga ya Israel.

Chanzo: Bbc