Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Misri, Uturuki watifuana kupata nafasi Sudan

Misri, Uturukiiii Misri, Uturuki watifuana kupata nafasi Sudan

Thu, 19 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakuu wa mashirika ya kijasusi ya Uturuki na Misri wamefanya ziara kwa kupishana kidogo tu nchini Sudan suala ambalo linaonesha wazi jinsi nchi hizo mbili zinavyoshinda kuwa na ushawishi katika nchi hiyoya Afrika.

Shirika la habari la Tasnim limeripoti kuwa, wiki mbili zilizopita, Abbas Kamel, mkuu wa ujasusi wa Misri, alielekea Khartoum, mji mkuu wa Sudan, na kukutana na maafisa wa kijeshi wa nchi hiyo na mara baada ya ziara hiyo, mkuu wa shirika la kijasusi la Uturuki, Hakan Fidan naye alifunga safari kuelekea Sudan ambako alikutana na maafisa wa kijeshi na usalama wa nchi hiyo.

Duru za usalama za nchi za Kiarabu zimesema kuwa Misri ina wasi wasi kuhusu harakati na upanuzi wa vituo vya kijeshi, kisiasa na kiuchumi vya Ankara nchini Sudan.

Gazeti la Al-Arab la mjini London limeandika kuwa mlolongo wa ziara za maafisa wa nchi hizo mbili nchini Sudan unaashiria kukua kwa diplomasia ya kijasusi katika eneo hilo. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Misri inafahamu vyema maendeleo ya hivi karibuni katika uhusiano wa Sudan na Uturuki, na haijaridhishwa na kujitanua Uturuki katika Bahari ya Shamu. 

Licha ya kujitokeza ishara za kisiasa za maelewano kati ya Cairo na Ankara, ambayo yalipelekea Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kukutana mjini Doha mwezi Novemba mwaka jana, lakini bado uhusiano wa nchi hizo mbili umeshindwa kurejea katika hali ya kawaida kama zamani. 

Sababu ya mkwamo uliopo baina ya nchi mbili za Uturuki na Misri, kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya gazeti la Al-Arab, ni kwamba bado kuna kesi ambazo hazijatatuliwa kati ya pande hizo mbili na huenda Sudan ni moja ya kesi hizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live