Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Misri, Ethiopia na Sudan waanza tena mazungumzo kuhusu bwawa la Ethiopia

Misri, Ethiopia Na Sudan Waanza Tena Mazungumzo Kuhusu Bwawa La Ethiopia Misri, Ethiopia na Sudan waanza tena mazungumzo kuhusu bwawa la Ethiopia

Mon, 28 Aug 2023 Chanzo: Voa

Misri, Ethiopia na Sudan Jumapili wameanza tena mazungmzo ambayo yamekuwepo kwa miaka kadhaa kuhusiana na bwawa lenye utata lililojengwa na Ethiopia kwenye mto Nile.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, mazungumzo hayo yamerejelewa baada ya rais wa Misri Abdel Fattah el Sissi na waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed kusema mwezi uliopita kwamba wanalenga kufikia makubaliano ndani ya miezi 4, kuhusu operesheni za bwawa hilo la Ethiopia Renaissance lililogharimu dola bilioni 4.6 za kimarekani na lililopo kwenye mto wa Blue Nile.

Blue Nile unakutana na White Nile karibu na mji mkuu wa Sudan, Khartoum, kabla ya kuendelea upande wa kaskazini kuelekea Misri, na hatimaye kwenye bahari ya Mediterranean. Misri inahofia kwamba bwawa hilo huenda likaathiri shughuli zake iwapo litaendeshwa bila kuzingatia maslahi yake.

Taifa hilo la kiarabu lenye idadi kubwa zaidi ya wakazi hutegemea maji ya Nile kwa ajili ya kilimo, ambapo chanzo cha asilimia 85 ya maji yake ni Ethiopia.

Chanzo: Voa