Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mimi ndiye mhalifu mkuu, niadhibiwe: Museveni

State004pix Data 1140x640 Mimi ndiye mhalifu mkuu, niadhibiwe: Museveni

Mon, 10 Oct 2022 Chanzo: Dar 24

Museveni amejivunia kuwa kiongozi mkuu wa uongezaji thamani wa bidhaa zinazozalishwa nchini Uganda, huku akikabiliwa na upinzani wa umma baada ya kuiunga mkono Uganda Vinci Coffee Company Limited, kuchukua mchakato wa kuongeza thamani kwa kahawa yote ya Uganda kwa ukiritimba.

Akitoa hotuba yake kwenye sherehe za Uhuru wa Kololo Oktoba 9, 2022, Rais Museveni alionesha kutofurahishwa na kile alichowaita wahusika wa siasa, waliopinga wazo lake la kukuza uongezaji thamani nchini na kusema kama ni uhalifu basi yeye ndiye mshukiwa wa kwanza hivyo aadhibiwe.

Amesema, “Vimelea kama vile Monitor hushambulia mipango ya serikali mfano wa hivi majuzi walisema maelezo yao nayanukuu “dili ya kahawa inanuka, wakosaji hawataadhibiwa,” niliyesimama hapa mimi ndiye mkosaji, njoo uniadhibu kwa maneno mengine, ninafanya uhalifu kujaribu kuongeza thamani ya kahawa yetu?.”

“Nchini Uganda, tumekuwa na vita na watendaji wa kisiasa kuhusu kuongeza thamani, kila kitu kinapatikana kutoka nje bado malighafi zinapatikana na angalau tumeanza kuzalisha posho zetu wenyewe, maziwa yaliyosindikwa, mbolea na baadhi ya nguo,” aliongeza Rais Museveni.

Desemba 15, 2021 imepangwa kuwa siku ya utolewaji wa uamuzi wa shitaka la Kahawa Mahakamani nchini humo, baada ya sehemu ya mawakili akiwemo Henry Byansi na Michael Aboneka kuiomba mahakama itangaze makubaliano yaliyotiwa saini kati ya serikali na muuzaji kahawa kinyume cha sheria.

Walalamikiwa katika kesi hiyo, ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kiryowa Kiwanuka, na Uganda Vinci Coffee Company Limited huku nchi hiyo ikiwa inaongoza kwa kuuza kahawa barani Afrika, na jumla ya uzalishaji wake wa kahawa inawakilisha takriban asilimia tano ya uzalishaji wa zao hilo Duniani.

Rais Museveni, na wataalam wa sera katika Wizara ya Fedha na UCDA, wana uhakika kwamba nchi hiyo inaweza kupata pesa zaidi kwa kusindika kahawa yake yote, kuitumia nchini au kuuza kahawa iliyosindikwa kwenye soko la kimataifa.

Hata hivyo, baada ya majadiliano makali na shinikizo kutoka kwa wananchi, Bunge lilichukua uamuzi wa kusitisha mpango huo, wa mkataba wenye utata wa kahawa, habari ambazo zilipokelewa kwa furaha huku baadhi ya wadau wakilipongeza Bunge la 11 kwa kusimama na Waganda.

Chanzo: Dar 24