Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Milipuko yatikisa jiji wa Khartoum

Karthouom Sudan Milipuko yatikisa jiji wa Khartoum

Fri, 23 Jun 2023 Chanzo: Voa

Milipuko ilitikisa miji mkuu wa Sudan wa Khartoum siku ya Alhamisi, miezi miwili zaidi baada ya mapigano kuzuka kati ya majenerali hasimu nchini, huku kila upande ukimshutumu mwingine kwa mashambulizi dhidi ya raia.

Mashahidi waliko mashariki mwa mji mkuu waliripoti mashambulio ya bunduki, huku wengine waliko katika vitongoji vya kaskazini wakisema mashambulio makali ya mizinga kutoka kambi ya jeshi yalitikisa kuta za nyumba.

Mashambulizi ya angani kwa mara nyingine tena yameathiri maeneo kadhaa ya jiji la Khartoum.

Huko Omdurman, mji pacha na Khartoum ulioko ng'ambo ya pili ya Mto Nile, "mashambulizi makali ya mabomu ya anga na silaha za kushambulia ndege" yaliendelea “kwa zaidi ya saa mawili mfululizo", shahidi mmoja aliliambia shirika la habari la AFP.

Katikati ya mji wa Khartoum, walioshuhudia walisema mapigano yalizuka mitaani huku "ndege za kijeshi zikiruka juu" katika eneo ambalo "lilikuwa shwari kwa siku kumi."

Nchi hiyo ya Sudan inayokumbwa na vita, mji mmoja kwenye mto wa Blue Nile umekuwa mahala watu wanakimbilia ili kuepuka mapigano, lakini waathirika wanaoishi katika mji huo wanavumilia msongamano, magonjwa yanayoenea na njaa inayojitokeza.

Watu wengi wamepata hifadhi katika kambi za muda zilizowekwa katika shule, mabweni ya chuo kikuu na majengo mengine huko Wad Madani, mji uliyoko kwenye ukingo wa Blue Nile katika eneo la kilimo cha pamba katika jimbo la Al-Jazirah

Chanzo: Voa