Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Milipuko yaripotiwa eneo la Morocco huko Sahara Magharibi

Milipuko Yaripotiwa Eneo La Morocco Huko Sahara Magharibi Milipuko yaripotiwa eneo la Morocco huko Sahara Magharibi

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Milipuko minne Jumamosi jioni kwenye mji wa Smara kwenye eneo linalodhibitiwa na Morocco la Sahara Magharibi umeua mtu mmoja na kujeruhi wengine watatu kulingana na mamlaka za kieneo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, taarifa iliyotolewa na mamlaka imesema kwamba milipuko hiyo iliharibu nyumba mbili, bila kutoa maelezo zaidi.

Morocco inachukulia Sahara Magharibi kuwa ni eneo lake, lakini kundi la Polisario Front linaloungwa mkono na Algeria linataka uhuru wa eneo hilo. Novemba mwaka 2020, Polisario Front lilisema limeanza tena mapigano, ingawa Umoja wa Mataifa ulisema kwamba hayakuwa yenye nguvu.

Morocco imesisitiza kwamba inachoweza kufanya ni kutoa uhuru wa kujitawala kwa eneo hilo na wala siyo uhuru kamili kama unavyodaiwa na Polisario na Algeria.

Chanzo: Bbc