Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mikakati ya rais Ndayishimiye ya kukabiliana na Covid-19

NDAYI Mikakati ya rais Ndayishimiye ya kukabiliana na Covid-19

Thu, 2 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka nchini Burundi imetangaza kutumia njia za aina yake kukabiliana na mlipuko wa virusi vya corona na kuachana na namna ambavyo taifa hilo lilivyokuwa linakabiliana na janga hilo wakati wa utawala uliopita.

Katika hotuba yake mara baada ya kuapishwa urais, Bwana Evariste Ndayishimiye alitangaza hatua zifuatazo za kupambana na corona ikiwa ni pamoja na hatua maalum kuhusu matumizi ya sabuni.

Mosi ni kuhakikisha kuwa idadi kubwa ya watu wanapata sabuni, gharama ya bidhaa hiyo inabidi ipungue kwa asilimia 50 huku serikali ikifidia nusu yake ili viwanda visipate hasara. Aidha mtu yeyote atakayepatikana anauza sabuni kwa magendo kutoka Burundi atadhaniwa kuwa anasaidia kumbaza virusi vya corona na hivyo kuwajibishwa ipasavyo," alisema rais. Katika miji yote, gharama ya maji itapunguzwa mpaka virusi vya corona vitakakapoisha. Mtu yeyote atakayeonyesha dalili za ugonjwa wa corona atatakiwa kufika hospitalini na atatakiwa kupimwa na kuhudumiwa bure.

Kama mlipuko utaisha kila mtu atatakiwa kupima virusi hivyo.

Mabadiliko hayo yamekuja mara tu rais mpya Bwana Ndayishimiye alipoingia madarakani, licha ya kwamba wakati wa kampeni za urais wake picha mikusanyiko ya maelfu ya watu waliokusanyika katika mikutano ya kampeni za kisiasa ziliibua wasi wasi mkubwa wa kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya corona kabla ya taifa hilo kufanya uchaguzi tarehe 20 Mei mwaka huu. Unaweza pia kusoma:

Nani anaiongoza Burundi baada ya kifo cha Nkurunziza?

Mikutano mikubwa ilishuhudiwa katika nchi hiyo ambapo tume ya taifa ya uchaguzi nchini humo ilitoa sabuni na ndoo kwa wagombea wa uchaguzi ilivitumiwe na wafuasi wao kunawa mikono wakati wa kampeni , wakati mmoja pia kemikali za kuua vimelea pia zilitumika.

Lakini "idadi ya watu waliohudhuria mikutano hiyo ilikuwa kubwa mno kiasi cha kutotoshwa na maji na vitakasa mikono vilivyokuwepo ", mmoja waliohudhuria mkutano wa kampeni katika mkoa wa Kirundo aliiambia BBC.

Mikutano mikubwa ya Kampeni za uchaguzi yaibua hofu ya maambukizi ya virusi vya corona.

Katika mitandao ya kijamii baadhi ya watu walielezea hofu zao huku wakiishutumu serikali kwa kuhatarisha maisha ya watu:

'Hakuna tisho la kutosha kuahirisha uchaguzi'

Serikali ya Burundi ilifunga mipaka yake ili kuzuwia kusambaa kwa virusi, na kuruhusu shehena za malori ya mizigo tu kuingizwa nchini kutoka mataifa jirani.

Ndani ya nchi, watu wameshauriwa kutosalimiana kwa mikono na kunawa mikono mara kwa mara, na maisha yanaendelea kama kawaida.

Serikali ilisisitiza kuwa kuwa bado hakuna tisho la kuifanya iahirishe uchaguzi mkuu.

Alipotazama picha za mikutano ya kisiasa nchini , Dkt Olivier Manzi mtaalamu wa mamgonjwa ya maambukizi aliiambia BBC kuwa hayo ni maeneo yanayoweza kuwa kitovu cha maambukizi ya virusi vya corona.

Dkt. Manzi ambaye anafanya kazi katika Shirika la Afya Duniani (WHO), ameiambia BBC kuwa mikusanyiko hiyo ni maeneo yanayosambaza kwa kasi virusi vya corona.

"Kwa mfano nchini Senegal, kulikua na visa vichache mwanzoni lakini baada ya mikusanyiko mikubwa ambayo ilitokea idadi ya visa ilipanda haraka, hii pia imeshuhudiwa katika baadhi ya mataifa mengine " - anasema Daktari Manzi.

Serikali ya Nkurunziza iliamua kuwatimua wafanyakazi wa Shirika la afya duniani(WHO) kutoka Burundi, wakati ulimwengu ukikabiliana na janga la Covid-19.

Taarifa kuhusu visa vya maambukizi ya virusi vya corona zimekua nadra sana kutolewa na serikali ya Burundi.

Iwapo mikakati inayowekwa sasa na utawala wa Bwana Ndayishimiye itasaidia kuzuwia maambukizi, ni jambo la kusubiri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live