Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miili zaidi yapatikana baada ya mafuriko makubwa DR Congo

Miili Zaid Drc Miili zaidi yapatikana baada ya mafuriko makubwa DR Congo

Thu, 15 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wafanyakazi wa uokoaji wamepata miili 11 zaidi ya watu walifarikikufuatia mafuriko ya Jumanne usiku katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kinshasa.

Miili hiyo ilipatikana kaskazini mwa wilaya ya Mont-Ngafula ya mji ambapo nyumba nyingi zimejengwa kwenye maeneo ya milimani ambayo yalikumbwa na maporomoko ya ardhi.

Mafuriko hayo yametajwa kuwa mabaya zaidi kuwahi kushuhudiwa kwa miaka mingi katika jiji hilo.

Takriban kaya 30,000 zimeathirika, huku nyumba 280 zikisombwa na maporomoko ya ardhi.

Rais FĂ©lix Tshisekedi anatarajiwa kurejea nchini siku ya Alhamisi kutoka Washington baada ya kufupisha ushiriki wake katika Mkutano wa Marekani na Afrika.

Idadi rasmi ya vifo ni 120 lakini mashirika yasiyo ya kiserikali yanasema zaidi ya watu 140 walikufa.

Uharibifu wa miundombinu ni mkubwa, huku wakazi wengi katika mji mkuu wakikabiliwa na kukatika kwa maji na umeme.

Siku ya Jumanne viongozi waliamuru kubomolewa kwa majengo yaliyojengwa kwenye maeneo yaliyohatarini kuporomoka na yale yaliyojengwa kwenye mfumo wa mifereji ya maji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live