Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miili zaidi yaopolewa baada ya lori kusombwa na mafuriko Kenya

Mafuriko Nchini Kenya: Basi Lililojaa Abiria Lasombwa Na Maji Yenye Mafuriko Miili zaidi yaopolewa baada ya lori kusombwa na mafuriko Kenya

Sat, 27 Apr 2024 Chanzo: Bbc

Miili mingine mitatu imeopolewa kutoka kwa Mto Kwa Muswii katika Kaunti ya Makueni Mashariki mwa Kenya baada ya lori lililokuwa likijaribu kuvuka mto uliofurika kusombwa na maji ya mafuriko.

Hii inafanya idadi ya vifo kutokana na tukio hilo kufikia 8, huku ripoti zikionyesha kuwa watu 10 zaidi hawajulikani waliko. Watu wengine 14 wameokolewa na kutibiwa.

Kulingana na taarifa za vyombo vya habari vya ndani watu hao walisombwa na mafuriko wakati wakielekea nyumbani kutoka soko la Yaitha.

Walioshuhudia tukio hilo wanasema Lori la kwanza lilifanikwa kuwavusha watu salama lakini Lori la pili lilishindwa na kusombwa na maji hayo.

Wakazi hao wamesema kuwa walikuwa wamepiga kambi kwenye kingo za mto huo tangu asubuhi, wakisubiri maji yapungue ili wavuke lakini maji hayo kadri muda ulivyozidi yalizidi kuongezeka.

Mvua kubwa inayonyesha kwa sasa katika maeneo tofauti nchini Kenya imewaathiri mamia ya watu awalioachwa bila makao.

Chanzo: Bbc