Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miili ya watu wanaoshukiwa kuwa wahamiaji yapatikana msitu wa Malawi

Miili Ya Watu Wanaoshukiwa Kuwa Wahamiaji Yapatikana Msitu Wa Malawi Miili ya watu wanaoshukiwa kuwa wahamiaji yapatikana msitu wa Malawi

Thu, 20 Oct 2022 Chanzo: BBC

Polisi wa Malawi wanachunguza vifo vya watu 10 wanaodhaniwa kuwa wahamiaji kufuatia kupatikana kwa miili yao katika hifadhi ya msitu katika wilaya ya kaskazini ya Mzimba.

Msemaji wa polisi alisema ugunduzi huo ulifanywa Jumatano asubuhi na kwamba kuna uwezekano miili zaidi itapatikana.

Polisi wanaamini kuwa miili hiyo "ina uwezekano mkubwa kuwa ni raia wa Ethiopia au somali," msemaji huyo alisema.

Wahamiaji mara nyingi huzuiliwa katika sehemu mbalimbali za nchi.

Baadhi wamefikishwa mahakamani na kufukuzwa nchini baada ya kupatikana na hatia ya kuingia Malawi kinyume cha sheria.

Maafisa wanasema wahamiaji wengi waliokamatwa nchini Malawi wanaitumia nchi hiyo kama njia ya kupita kuelekea Afrika Kusini, Ulaya au Marekani.

Chanzo: BBC