Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miili ya wahamiaji yapatikana pwani ya Mauritania

Mauritania Miili ya wahamiaji yapatikana pwani ya Mauritania

Tue, 14 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Mauritania inasema miili ya watu 16 wanaodhaniwa kuwa wahamiaji imepatikana katika pwani ya kaskazini mwa nchi hiyo.

Kugunduliwa kwa miili hiyo kwenye fukwe za Lagouera kunakuja wiki moja baada ya maiti 13 kupatikana kwenye boti katika eneo hilo hilo, karibu na mji wa Nouadhibou.

Tukio hili la hivi punde linaonekana kutokea baada ya boti yao kugonga mawe.

Hivi mkaribuni kumekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya watu wanaosafiri kutoka nchi jirani ya Senegal katika harakati za kufika katika Visiwa vya Canary nchini Uhispania.

Tangu Januari zaidi ya watu 23,000 wamefika huko kwa boti.

Chanzo: Bbc