Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miili ya vijana 4 yapatikana katika shamba linalomilikiwa na jeshi la KDF

 Miili Ya Vijana 4 Yapatikana Katika Shamba Linalomilikiwa Na Jeshi La KDF Miili ya vijana 4 yapatikana katika shamba linalomilikiwa na jeshi la KDF

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: Radio Jambo

Huzuni na wasiwasi vilitanda katrika eneo la Kamagut, kaunti ya Uasin Gishu Jumapili asubuhi baada ya miili ya vijana 4 wenye umri wa makamo kupatikana imetapakaa katika shamba la mahindi linaloaminika kusimamiwa na maafisa wa KDF kutoka kwa kambi ya jeshi ya Moi, mjini Eldoret.

Kwa mujibu wa taarifa za awali, vijana hao waliuawa kwa kuingia kinyume cha sheria katika shamba hilo la jeshi na kushambuliwa kwa kipigo hadi kufa na walinzi wa shamba hilo.

Naibu kamishna wa kaunti ndogo ya Turbo kama alivyonukuliwa na jarida la Nation.Africa alibaini kwamba vijana hao walikuwa wameingia katika shamba hilo kuokota mahindi yaliyosazwa baada ya mavuno lakini wakavamiwa na walinzi ambao ni wenyewe wa eneo hilo.

“Miili mitatu ya vijana ilipatikana Asubuhi Jumapili huku wa nne akifariki katika hospitali ambao wengine pia wanazidi kupata matibabu. Vijana hao wote walikuwa kati ya umri wa miaka 18 hadi 25,” kamishna huyo alisema.

Wenyeji hata hivyo wanahisi kwamba huenda vijana hao waliuawa kwingine na miili yao kutupwa huku, wengine wakisema kwamba ni kutokana na ugumu wa maisha ambao uliwasukuma vijana hao kuingia katika shamba hilo kujizolea mabaki ya mahindi baada ya mavuno.

Tayari maafisa wa KDF wakishirikiana na wenyeji wameanza msako katika shamba hilo pana ili kutafuta kama kuna miili ya wengine ambayo imetapakaa.

Chanzo: Radio Jambo