Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miguna ashauriwa kuvaa kama mwanamke na kuingia Kenya kwa njia za Panya

C271cd2839f4b596 Miguna ashauriwa avalie kama mwanamke na kuingia Kenya kupitia vichochoro Uganda

Wed, 17 Nov 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Mshairi wa Uganda Stella Nyanzi amemshauri Miguna Miguna kujaribu kutumia mbinu za magendo kuingia Kenya baada ya kukataliwa kwa mara ya tatu.

Kwa mujibu wa Nyanzi, alimshauri wakili huyo anayeishi Canada kupanda ndege itakayomfikisha nchi jirani ya Uganda, kisha ajikwatue kama mwanamke halafu aanze safari ya kuenda nyumbani Alisema badala ya kutumia mpaka wa Malaba, Miguna anaweza kupitia njia nyingi za vichochoro vilivyoko kati ya mataifa haya mawili Mtetezi wa haki za binadamu Stella Nyanzi amependekeza wakili Mkenya anayeishi Canada, Miguna Miguna kupenyeza Kenya akiwa amevaa kama mwanamke.

Nyanzi alimuonea huruma Miguna baada ya safari yake kutibuka kufuatia tahadhari iliyotolewa na serikali ya Kenya kwa mashirika ya ndege. Miguna alipaswa kuwasili Kenya Novemba 16 ila alizuliwa na Shirika la ndege la Ufaransa.

"Tutampokea vyema na kumpaka vipodozi, kunyoa ndevu zake na kuhakikisha uso wake umepakwa Copper Girl ili awe mweupe pepepe, tutamsonga nywele za Brazilian, tutamtafutia sidiria iliyojazwa pamba na kumpa rinda la kitenge avae, hatimaye tutampenyeza hadi Kenya kwa kutumia pikipiki," Nyanzi alitoa ushauri.

Ushauri wake, kama ilivyotarajiwa, ulishambulia utawala wa Ugandan wakati aliposema Miguna anaweza kuingia Kenya kwa kutumia vichochoro vya magendo ambako askari huwa wanakula hongo na kuwaruhusu watu kupita maeneo ya mpakani.

Kwa kifupi, Stella alipendekeza Miguna Miguna atumize nji za mkato na za kimagendo zinazoruhusiwa kiyume cha sheria ili ajifaidi.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke