Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miguna ajutia kumchokoza Raila, azomewa na Wakenya mitandaoni

28a50f9dcd8eac33 Miguna ajutia kumchokoza Raila, azomewa na Wakenya mitandaoni

Mon, 8 Nov 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Wakili Miguna Miguna amekuwa akimtupia maneno makali Raila Odinga na kuhoji kuhusu kuhitimu kwake katika tasnia ya uhandisi. Hata hivyo, Jumapili Novemba 7, cheche za Miguna kwa Raila zilitibuka baada ya kushindwa kuelewa ujumbe alioupakia mtandaoni.

Baada ya kuzuru mji wa Engineer katika Kaunti ya Nyandarua, Raila, ambaye ni mhandisi alipakia ujumbe kwenye mitandao yake ya kijamii uliosema "Engineer akiwa Engineer" Hata hivyo Miguna, hakuelewa ulivyomaanisha ujumbe huo na kujibu upesi akidai kiongozi huyo wa ODM alikosea kimaandishi Kwa muda mrefu sasa, Wakili Mkenya anayeishi Canada Miguna Miguna amekuwa akimrushia cheche kali za maneno, kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga.

Hata hivyo, Jumapili Novemba 7, Miguna aliambulia patupu alipojaribu kumshambulia Raila kwa maneneo. Wakati Raila aliokuwa Nyandarua kufanya kampeni ya ajenda yake ya Azimio la Umoja, Raila aluzuru wadi ya Engineer iliyoko kaunti ndogo ya Kinangop.

Raila alipakia ujumbe uliokuwa na picha kwenye ukurasa wake wa Twitter, uliosoma "an Engineer in Engineer" kumaanisha yeye ni mhandisi, aliyezuru eneo la mhandisi.

Miguna, kwa haraka alidakia na kujibu bila ya kuelewa alichomaanisha Raila na kudhanioa alikuwa amekosea kimaandishi.

"Ujumbe ulioandika una makosa kimaandishi. Hebu rekebisha kiingereza chako. Maandishi sahihi kwa Kiingereza ni: "an engineer is an engineer." Nawe sio mmoja wao," Miguna alisema.

Baadhi ya maoni yaliyotolewa na kuchapishwa na TUKO.co.ke:

Lilian Lillow alisema:

"Ukosoaji wako umetibuka, chuki zako zimezidi."

Evangeline Ngungi alisema:

"Hii ndiyo sababu tanafikiri kwamba wewe sio Mkenya. Kuna mahala panaitwa hivyo. Jua taifa lako vyema."

Manyara Stephen alisema:

"Kwani hujui kuna eneo fulani Nyandarua linaloitwa Engineer. Waona sababu serikali inataka ukae nchini mwako (Canada)."

Benson Musungu alisema:

"Wewe umechanganyikiwa. neno la kwanza mhandisi linamaanisha cheo, na neno la pili mhandisi linamaanisha mji uliko Nyandarua."

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke