Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miguna Miguna ashindwa kuwasili Kenya

91201 Pic+miguna Miguna Miguna ashindwa kuwasili Kenya

Thu, 9 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Nairobi, Kenya. Mwanasheria na mwanaharakati wa Kenya, Dk Miguna Miguna ameshindwa kuwasili nchini humo leo Jumatano Januari 8,2020 kutokana na kile anachokiita ni tahadhari (Red Alert) iliyotolewa na serikali ya Kenya kwa mataifa mbalimbali.

Dk Miguna alizuiliwa jana Uwanja wa Ndege wa Charles de Gaulle wa Ufaransa kwa sababu mamlaka za Kenya zilitoa angalizo kuhusiana na kusafirishwa kwa Dk Miguna kwenda Nairobi, Kenya.

Pia, alizuiwa kusafiri akiwa uwanja wa ndege wa Frankfurt huko Ujerumani kwa madai hayo hayo kwamba serikali ya Kenya imeyahadharisha mataifa mbalimbali kuhusu kumsafirisha kwenda Nairobi, Kenya.

Kwa mujibu wa mtandao wake wa Twitter, Dk Miguna alibainisha kwamba alishushwa kwenye ndege ambayo ilikuwa karibu kuondoka. Aliandika kwamba serikali ya Kenya ilitoa tahadhari kwa mashirika yote ya ndege kumsafirisha mpaka Kenya.

Hata hivyo, jana aliahidi kwamba leo Januari 8 saa 3 asubuhi atawasili Nairobi, Kenya kwa maanda kwamba tayari alipata ndege ya kumsafirisha mpaka Nairobi.

Mpaka majira ya saa 8 mchana, bado Dk Miguna alikuwa hajawasili Nairobi huku kukiwa hakuna taarifa zozote kutoka kwake wala mamlaka nyingine za Kenya.

Dk Miguna aliingia kwenye mgogoro na mamlaka za Kenya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2017 kwa kumuapisha Raila Odinga kama Rais wa watu wakati Rais aliyetangazwa na Tume ya Uchaguzi akiwa ni Rais Uhuru Kenyatta.

Hata hivyo Dk Miguna amekuwa mkosoaji mkubwa wa Rais Kenyatta pamoja na Raila baada ya wawili hao kukubaliana kumaliza tofauti zao na kuamua kuijenga Kenya pamoja, bila kujali tofauti zao za kisiasa.

Dk Miguna anadaiwa kubadilisha uraia wake na kuwa na uraia wa Canada ambako amekuwa akiishi tangu alipoondoka baada ya uchaguzi na mara kadhaa alijaribu kurudi Kenya lakini alikataliwa kuingia nchini humo.

Chanzo: mwananchi.co.tz