Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miezi mitatu ya vita nchini Sudan hali bado ni tete

Miezi Mitatu Ya Vita Nchini Sudan Hali Bado Ni Tete Miezi mitatu ya vita nchini Sudan hali bado ni tete

Fri, 16 Jun 2023 Chanzo: Voa

Mapigano hayo yamesababisha watu milioni 2.2 kuyakimbia makaazi yao wakiwemo watu 528,000 ambao wamekimbilia nchi jirani, linasema shirika la kimataifa la uhamiaji

Vita vya Sudan vimeingia mwezi wa tatu siku ya Alhamisi wakati idadi ya vifo ikifikia 2,000 na baada ya gavana wa jimbo hilo kuuawa katika jimbo la Darfur.

Tangu Aprili 15 jeshi linaloongozwa na Abdel Fattah al-Burhan limekuwa likipigana na vikosi vya wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF) vinavyoongozwa na aliyekuwa naibu wake, Mohamed Hamdan Daglo.

Mapigano hayo yamesababisha watu milioni 2.2 kuyakimbia makaazi yao, wakiwemo watu 528,000 ambao wamekimbilia nchi jirani, linasema shirika la kimataifa la uhamiaji.

Katika utabiri wetu, hatukutegemea vita hivi vingeendelea kwa muda mrefu, alisema Mohamad al-Hassan Othman, miongoni mwa raia zaidi ya milioni moja, ambao wamekimbia mapigano haya katika mji mkuu Khartoum.

Kila kitu katika maisha yetu kimebadilika, aliliambia shirika la habari la AFP. Hatujui kama tutarudi nyumbani au tunahitaji kuanza maisha mapya.

Chanzo: Voa