Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Microsoft kuleta intaneti Afrika kupitia satelaiti

Satelite Afrik Aaaaaa Microsoft kuleta intaneti Afrika kupitia satelaiti

Thu, 15 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kampuni ya Microsoft imetangaza leo mipango ya kuleta huduma za intaneti kupitia satelaiti kwa watu milioni 10, nusu yao wakiwa barani Afrika, kama sehemu ya juhudi za kuziba pengo la kidijitali na ulimwengu unaoendelea.

Katika mkutano na viongozi wa Afrika mjini Washington ukiongozwa na Rais Joe Biden, kampuni hiyo kubwa ya teknolojia imesema itaanzisha mara moja mradi huo wa satelaiti kwa kipaumbele cha kuleta intaneti kwa mara ya kwanza katika maeneo ya Misri, Senegal na Angola.

Rais wa Microsoft Brad Smith amesema kampuni hiyo imevutiwa na wahandisi wake wa Nairobi na Lagos.

Smith amesema barani Afrika hakuna uhaba wa vipaji, lakini kuna uhaba mkubwa wa fursa. Viongozi 49 wa Afrika wanahudhuria mkutano huo wa kilele wa siku tatu ambao ulianza hapo jana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live