Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mhubiri mbaroni kwa kumlewesha muumini kisha kumbaka

HUKUMU Mhubiri mbaroni kwa kumlewesha muumini kisha kumbaka

Wed, 26 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya magharibi ya Ndola nchini Zambia imemtita hatiani Mhubiri Gellion Jones (28) kwa kumtendea unyanyasaji wa kingono msichana mwenye umri wa miaka 17 wakati wa sala kwa kumwekea kilevi na kumwingilia kwa siku tatu mfululizo.

Jones, ambaye ni mhubiri wa eneo la Kopaland, anadaiwa kumtendea unyanyasaji wa kingono msichana mwenye umri wa miaka 17 kwa siku tatu ndani ya jengo la kanisa mwezi Septemba mwaka jana.

Katika ushahidi wake, muathirika aliiambia mahakama kuwa siku ya tukio, alikuwa na mpenzi wake katika Kituo cha Polisi cha Kambeba, ambapo mpenzi wake alikuwa amezuiliwa kwa tuhuma za unyanyasaji.

Alisema baada ya kulala usiku katika kituo cha polisi, alikwenda nyumbani kwa mhubiri kwa hofu ya wazazi wake baada ya kuwa na mpenzi wake, ambaye wazazi wake hawakumkubali.

Muathirika alidai kuwa wakati yupo katika nyumba ya mhubiri, alipewa maji ambayo yalimfanya awe na mshawasha baada ya kuyanywa. Muathirika alidai pia kuwa Jones alimpa kinywaji hicho kila siku kwa siku tatu hadi alipookolewa kutoka mahali hapo siku ya tatu, wakati wazazi wake walipoenda kumtafuta.

Katika utetezi wake, Jones alikana kufanya kosa hilo akidai kuwa wakati alikamatwa, polisi pamoja na muathirika walitembelea kanisa, ambapo tukio linadaiwa kutokea. Alisema wakati muathirika alipoambiwa kuwaonyesha polisi chumba ambapo anadaiwa kufanyiwa unyanyasaji wa kingono, alishindwa kufanya hivyo.

Lakini Hakimu Veronica Sikwangala alimkuta Jones na hatia akisema anaamini ushahidi wa muathirika hasa kwa kuwa mama yake aliiambia mahakama kuwa mtoto wake alitoweka kutoka nyumbani tangu wakati kosa linadaiwa kutokea. Hakimu Sikwangala hata hivyo, alisema hana uwezo wa kutoa hukumu na atampeleka Mahakama Kuu kwa ajili ya hukumu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live